Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya Airtel yatosha.
• Ni washindi wa shilingi milioni moja wa wiki ya kwanza na ya pili ya promosheni
Jumapili 28 julai 2013, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaa na kuwazawadia washindi 14 wa kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kupitia huduma ya Airtel Money.
Washindi hawa wamepatikana kupitia droo ya wiki ya kwanza na ya wiki ya pili ambapo jumla ya washindi 14 kutoka katika mikoa mbalimbali ya nchi walipatikana na hatimaye kukabithiwa pesa zao
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa Kanda Mkoani Arusha bwana Stephen Akyoo alisema” leo tunayofuraha kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali na kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia huduma za Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali.
nae Meneja Uhusiano wa Airtel Akitangaza majina ya washindi hao bwana Jackson Mmbando alisema "washindi wetu wa wiki ya kwanza na ya pili ni pamoja na Hawa Said Mkazi wa Mtwara, John Masawe mkazi wa singida, Joseph Emmanuel Nchimbi Songea, Rosemary Michael na John Masanja kutoka Tabora , Zuhura Sabuni kutoka Lindi, Balistus mambo kutoka Moshi, Robert Faustine kutoka Arusha , Frank Ladislaus na Paulina Michael kutoka Sengerema Mwanza, Flavian Adamson Malilo kutoka Katavi, Jacob Muhole kutoka Dodoma, Singodi Severin kutoka Kagera na Ephrasia Thadeo kutoka Ngara.
Ili kushiriki mteja anatakiwa kupiga kupiga *149*99# na kununua kifurushi cha huduma ya Airtel yatosha cha siku, wiki au mwezi na kuunganishwa mojakwamoja kushiriki kwenye promosheni na kupata nafasi ya kushinda nyumba au pesa taslimu shilingi milioni moja kila siku.
Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Robert Justine moja kati ya washindi anayetokea mkoani Arusha alisema” nimefurahi sana kuwa mshindi wa promosheni na ntaendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha ili kuendelea kufaidika na huduma hii na kupata nafasi ya kushinda nyumba. Natoa wito kwa watanzania kutumia huduma hii na kuhakikishia hata wao wananafasi ya kushinda kama mimi nilivyoweza leo kukabithiwa shilingi milioni moja kwa kutumia tu huduma ya Airtel yatosha.
Promosheni ya Airtel yatosha bado inaendelea kwa mienzi mitatu hadi hapo mwishoni mwa mwenzi wa tisa ambapo mbali na zawadi za pesa taslimu wateja pia wanapata nafasi ya kujishindia nyumba 3 zilizopo kigamboni jijini Dar es saalam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.