Familia ya mwanariadha
mlemavu nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius, wameshstushwa na picha
zilizofichuliwa za bafu alimomuulia mpenzi wake mnamo mwezi Februari.
Pistorius atafikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana |
Shirika la habari la
Uingereza la Sky, mnamo Ijumaa, lilionyesha picha za kuogofya zinazoshukiwa
kuwa za bafu ambalo mpenzi wa Pistorius Reeva Steenkamp, aliuawa.
Bwana Pistorius mwenyewe anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake, kupitia mlango wa bafu alimokuwa , alisema alidhani kuwa alikuwa mwizi aliyevamia nyumba yake.Polisi walisema kuwa wamechukizwa mno na kufichuliwa kwa picha hizo.
Anatarajiwa kufikishwa
mahakamani kwa hatua ya mahakama mwanzo kutathmini kesi siku yake Jumanne.
Pistorius ni mwanariadha
mlevamu asiye na miguu yake miwili ingawa hukimbia kwa miguu bandia au vyuma.
Alishiriki michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana.
''Familia ya Pistorius
ilimuunga mkono alipokuwa anajiandaa kufikishwa mahakamani , alisema mjomba
wake,'' Arnold Pistorius.
''Tunaamini maneno
yake , tunampenda na tutamuunga mkono kwa kila hatua ya kesi hii,''alisema
Mjombake Pistorius. "tumeshtushwa na
picha hizi za ajali iliyotokea nyumbani kwa Oscar."
Msemaji wa polisi
ameelezea kuwa polisi wanachunguza nani aliyefichua picha hizo .
''Kitendo hiki
hakikuhitajika na kimetuudhi kweli. Hatujui picha hizi zimetoka wapi,'' alisema
polisi huyo.
Pistorius atafikishwa
mahakamani Jumanne kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana, kufuatia
kukamatwa kwake, kuhusu mauaji ya Steenkamp.
Kesi hiyo inatarajiwa
kuakhirishwa kwani uchunguzi wa polisi ungali unaendelea.
Pistorius ameajiri
baadhi ya mawaklili shupavu nchini Afrika Kusini kumtetea.
Anasema kuwa alimpiga
risasi Bi Steenkamp kupitia mlango wa choo kimakosa baada ya kudhani kimakosa
alikuwa mwizi. Hata hivyo, viongozi
wa mashtaka wanasema kuwa alimuua kwa maksudi baada ya wawili hao kugombana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.