ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 4, 2013

WAZIRI MKUU ALIPOKOSHWA NA MAZURI YALIYOPO BUJORA

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa wiki alifungua Tamasha la ngoma za jadi kwa kabila la Wasukuma lijulikanalo kwa jina la Bulabo na hapa pichani alikuwa akitembelea viunga mbalimbali vya vivutio vilivyopo eneo la makumbusho Bujora Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.


Padre Fabian Mhoja (aliyenyoosha mkono) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Katibu wa CCM mkoa pamoja na Naibu Waziri wa nishati na Madini walipotembelea makumbusho ya Bujora. 


Ramani ya Sukuma land ambayo ilikuwa ikitolewa ufafanuzi.


Watemi walikuwa wanamichezo yao inayowaweka pamoja na moja kati ya michezo hiyo ni mchezo wa bao.


Bao lenyewe.


Hivi unajua historia ya jina la eneo la Buhongwa lililopo jijini Mwanza? Ni kwanini viongozi hawa walicheka?


Hesabu za watu wa kabila la sukuma zilikuwa zikiishia namba 10, na uhesabu wa kila rika ulitofautiana watoto walikuwa na mtindo wao halikadhalika akina baba, mama, wazee na watemi.


Tizama kwa umakini utaona rika na mitindo ya uhesabu.


Crew ya Viongozi.

'Anayesema ni maadui yampasa kutafakari zaidi, wanajuana kwa vilemba hawa...' Ni mwenyekiti wa sasa CCM Mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo (kulia) na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe. Mabina (kushoto) ambapo kamera hii iliwanasa wakiwa pamoja wakishea aidiaz' kwa kila linanalojiri eneo la tukio na wakitumia zaidi ya safari nzima ya mizunguko kuvinjari vivutio vya Bujora kwa mazungumzo ya pamoja.


Picha iliyosheheni yote yaliyoko himaya ya hifadhi za Sukuma.


Tulimaliza ziara kwa kula chakula asili ya watu wa kabila la Wasukuma.
Nyama, viazi aka manumbu, makande ya mbaazi, wali, maziwa ya mgando, mlenda ..... na mengine yeeeeh!! 


Clouds Tv ilikuwepo eneo la tukio.


Kanisa la Bujora lenye hifadhi za kumbukumbu ya watu wa kabila la Sukuma.


Kila kitu hapa ni jadi.


G. Sengo hekaluni.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. I rеally liκe ωhat you guyѕ aгe usually up too.
    Such cleѵer woгk and reporting! Keep up the
    very gоod ωorks guys І've added you guys to my personal blogroll.

    Feel free to surf to my site Evaluate resort charges

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.