Na. Shomar Binda
Musoma.
Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha ya utoaji elimu katka Masuala mbalimbali katika Jamii,kuibua changamoto na kusaidia Makundi yasiyojiweza ya Jamii Information Network (JIN) inatarajia kuendesha kongamano la vijana mjini hapa mwaka huu wa 2013.
Picha Mkurugenzi wa Asasi ya Jamii Information Network (JIN) Augustine Mgendi. |
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Musoma,Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Augustine Mgendi amesema Kongamano hilo linatarajia kufanyika huku likiwakutanisha Vijana zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za Mjini hapa ambapo linalenga kuwajengea stadi za kujitambua,kujiamini na kujithamini.
Alisema katika Kongamano hilo vijana hao watafundishwa kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika makuzi yao lakini pia kuhamasisha Vijana kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi,kujifunza mbinu za Ujasirimali,dhana ya kujiajiri na Changamoto zake vijana kujenga Uzalendo,kupambana na Umaskini,Rushwa ,Kuepuka Mimba za Utotoni katika Jamii.
‘Nadhani Vijana bado wanachangamoto kubwa sana katika kufanikisha ndoto zao na hii ni fursa pekee kwa Vijana kujifunza Mbinu mbalimbali maana tutakuwa na wataalam ambao wamebobea katika mambo hayo ili kutoa Mwanga kwa Vijana wetu ” alisema Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Shule zitakazoshiriki Kongamano hilo zitatajwa baadaye baada ya Mambo kadha wa kadha kukamilika
“Ni Shule kumi zitakazoshiriki na mambo yakiwa tayari tutawafahamisaha ni shule gani ambazo tutakuwa nazo” alisema Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi huyo alisema kuwa watakuwepo wataalamu mbalimbali watakaohusika kutoa mafunzo katika Kongamano hilo huku akisema kuwa Vijana ndiyo nguvu kubwa ya Taifa kwasasa hivyo wanahitaj miongozo ya Kimaisha katika kujitambua
Kongamano hilo ambalo litakuwa linafanyika kila Mwaka litakuwa na kauli mbiu mbalimbali ambapo alisema kwa Mwaka huu litakuwa na Kauli mbiu ya “Jitambue Kijana” ambapo alisema kuwa Kongamano hilo litawasaidia Vijana wengi Kujitambua kutokana na Changamoto zinazowakabili kwasasa.
“Tunatarajia Kongamano hili liwe linafanyika kila Mwaka ili kutoa elimu na mwongozo wa kimaisha kwa vijana na kwa kuanza mwaka huu kauli mbiu yetu itafahamika kama Jitambue Kijana hii ni kutokana na vijana wengi kutofikia Malengo yako kutona na Changamoto zilizopo”alisema Bw Mgendi
Mbali na Kongamano hilo taasisi ya Jamii Information Network ambayo hufanya shughuli zake mkoa wa Mara inatarajia kutoa elimu mbalimba mkoani Mara ili jamii huska kwenda na wakati kutokana asilimia kubwa ya Watanzania kuishi vijijini ambapo vyombo vya habari kufika inakuwa tabu.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa Taasisi hiyo inatarajia kutumia wanahabari mkoani Mara kuibua changamoto mbalimbali zilizopo vijijini ili kuziweka bayana na kufanya vipindi mbalimbali kutoka Vijijini ambavyo alisema vitaibua Changamoto zilizopo huko.
Katika kufanikisha Kongamano hilo Mkurugenzi huyo ameyaomba Mashirika mbalimbali kujitokeza kufadhili Kongamano hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa wa kuwajenga Vijana hasa mkoani Mara.
“Mimi nayaomba mashirika mbalimbali kujitokeza ili kufanikisha Kongamano hilo maana najua litakuwa msaada mkubwa sana kwa Vijana ambapo kwa njia moja au nyingne litaweza kubadili fikra za vijana wanapomaliza masomo yao’ alimalizia Mkurugenzi huyo.
Nguvu kazi ya taifa lolote duniani ni vijana,hivyo wasipoandaliwa vizuri leo,kesho watakuwa bomu ambalo litakapolipuka litaangamiza taifa lote.Waafrika wanayo methali isemayo “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”,hivyo kama tunahitaji kuwa na kizazi bora chenye maadili,uzalendo na uwajibikaji tuanze kuwaandaa vijana sasa kisaikolojia,kimaadili na kimtazamo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.