ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 8, 2013

SERIKALI MMELIONA DARAJA HILI?

Wakati serikali ikiahidi kukamilisha ujenzi wa madaraja yapatayo 10 sehemu mbalimbali nchini huku ujenzi na ufunguzi wa madaraja hayo ukiendelea kufanyika hali iko hivi katika daraja la Sukuma lililopo katika barabara kuu inayounganisha vijiji vya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Daraja hili mbao zake zimesagika kabisa kiasi cha kufanya magari yanayopita kutumia daraja hili muhimu kupita kwa mwendo wa kusuasua yakihofia kukumbwa na maafa. 

Mbao zilizo chomoka zimeegeshwa tu, mawe yametumika kuziba mashimo ya uwazi kati ya nondo na nondo hii ni hatari si kwa magari tu bali hata kwa waendao kwa miguu hali inayosababisha hata waendeshao baskeli kushuka na kuzikokota baiskeli zao wakihofia usalama wao.

Shuhudia hali halisi ya daraja la Sukuma wilayani Magu, daraja ambalo hutumiwa na magari makubwa yabebayo tani na tani za mazao ya chakula pamoja na pamba, mbao zilizochoka zimeegeshwa tu bila misumari, 

Hili ndio daraja la Sukuma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.