ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 8, 2013

BREAKING NEWS: MWANDISHI WA RADIO KWIZERA ISSA NGUMBA AKUTWA AMEUAWA PORINI


MWANDISHI wa Habari wa kituo cha Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa Ngumba (45) ameua kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto huku simu zake mbili na Bastola iliyotumika kumshambulia ikiacha kando ya mwili wake porini.

Habari zilizopenyezwa kutoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi wa mkoa huo Frasser Kashai, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deo Sonkolo zimedai kuwa mwandishi huyo amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu ambao hawajajulikana.

Akizungumza na kwa njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na waandishi habari wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia uchunguzi wa Daktari Primus. 

Issa Ngumba (45)
Mwili wa marehemu umepatikana leo katika pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha Muhange, wilayani humo majira ya asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tokea siku ua Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya kutoonekana kwake.

Bastola iliyokutwa eneo la tukio imeokotwa ikiwa na risasi tano huku mifuko ya suruali ya marehemu ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi lake bado linangoja taarifa ya uchunguzi wa daktari sanjari na taarifa ya awali ya uchunguzi wa jeshi hilo toka eneo la tukio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.