|
Kocha Kim
Poulsen amekiri kuwa Stars kuweka kambi yake jijini Mwanza hakika lilikuwa ni
wazo sahihi kwani hamasa imeongeza kwa
wachezaji wake na hata walimu nao wanaahidi kuhakikisha wanacheza kufa na
kupona kwenye michuano hiyo kwa nia ya kuiletea sifa nchi ya Tanzania. Haya yamejiri kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa kikosi chetu kinachoelekea Kampala nchini Uganda hapo kesho.
|
|
Mwakilishi wa Vilabu Mkoa wa Mwanza kwenye
Mkutano Mkuu wa TFF Taifa Bw. John Kadutu (pichani mwenye miwani) licha ya kusema kuwa MZFA imejipanga
kuhakikisha mpira Mkoa wa Mwanza unakua kwa kasi na kuzalisha wachezaji wengine
kwa maslahi ya Timu za Taifa na vilabu mbalimbali pia alikuwa na nyongeza hii
kwa mashabiki kuelekea nchini Uganda kushuhudia michuano ya CECAFA |
|
Wachezaji a timu ya Taifa Tanzania bara pamoja na viongozi wakijadiliana na mastori kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa kikosi kinachoelekea Kampala nchini Uganda hapo kesho.. |
|
Baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars na viongozi wa soka Mwanza. |
|
Hewa safi ya Hoteli Tilapia....na kuchati kwa chati.... |
|
Refreshment kandokando ya ziwa Victoria |
|
Fun |
|
Old is good.. |
|
Yes we are... |
|
Bariz za hapa na pale.... |
|
Picha ya pamoja kati ya Kilimanjaro Stars na viongozi wa soka mkoa wa Mwanza MZFA |
WAKATI huo huo chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA)
kimewataka mashabiki wanaohitaji kwenda kuishangilia na kuipa hamasa timu ya
Taifa ya Kilimanjaro Stars inayoshiriki michuano ya CECAFA Challenge Cup 2012
inayotaraji kuanza jumamosi ya Novemba 24 mwaka huu Jijini Kampala nchini
Uganda kujitokeza kwa wingi na kuonana na uongozi wa MZFA kwaajili ya taratibu
za safari.
Kwa mujibu wa Katibu wa MZFA Bw.Nasbu Mabourk amesema
kuwa maandalizi ya taratibu za kupeleka
washabiki nchini Uganda kuishangilia Kilimanjaro stars katika kila
mechi itakazocheza zimekwisha kamilika na kuahidi kutoa gharama halisi ya
kwenda nchini humo siku ya ijumaa, ikiwa ni pamoja na ile ya hati ndogo ya kusafilia toka Idara
ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza
zitakazoratibiwa na MZFA kwa ajili ya kuwarahisishia mashabiki na
kuwaondolea usumbufu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.