ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 21, 2012

MAFUNZO YA UWAJIBIKAJI WA KIJAMII KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI NA VIONGOZI WA HALMASHAURI NA VIONGOZI WA WILAYA ZA UKEREWE NA MAGU KUMALIZIKA KESHO JIJINI MWANZA.


Bw. Asajile Lucas Mwambambale ambaye ni mwezeshaji wa semina hiyo akitoa ufafanuzi kuhusu uwajibikaji kwa jamii katika semina elekezi inayofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Victoria Palace iliyopo eneo la Capil Point mkabala na ofisi za TBC Taifa (Radio Tanzania) Mwanza. 


Semina hiyo inahusisha Watendaji wa Halmashauri na Viongozi wa Wilaya za Ukerewe na Magu ambapo humo ndani wakuu wa magereza kwa wilaya husika wamekutana hapa, Ma-OCD, Mahakimu, Wakurugenzi wa wilaya hizo, Wakuu wa idara za Halmashauri zote mbili na viongozi wa asasi za kiraia.


Mradi huu uko hapa nchini tangu mwaka 2009 ukifanya kazi katika wilaya za Magu, Ukerewe na Karagwe mkoani Kagera unafadhiliwa na Shirika la maendeleo la Swiden linalojihusisha na masuala ya uwajibikaji kwa jamii katika masuala ya Utawala bora, haki za binadamu na jinsia.


Usikivu ndani ya semina...


Washiriki wa semina elekezi inayofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Victoria Palace iliyopo eneo la Capil Point mkabala na ofisi za TBC Taifa (Radio Tanzania) Mwanza. 


Wakuu mbalimbali...


Wakuu mbalimbali na viongozi waliopo ndani ya chumba hiki cha mkutano.


Bw. Godfrey Wawa ambaye ni Meneja wa mradi wa Forum SYD-Tanzania akitoa darasa kwa washiriki juu ya nanna ya masuala ya uwajibikaji kwa jamii katika masuala ya Utawala bora, haki za binadamu na jinsia.


Wanasemina ndani ya mpango huu wengi wamekiri kunufaika na semina itolewayo, kwani wanasema kuwa kwao imekuwa ni fursa muhimu ya kukumbushana majukumu yao ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.








Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.