Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama
ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa
uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo
alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican
Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na
kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu
walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya
masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu
yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya
kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa
zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura
vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya
Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita
Tupe maoni yako
Continued
ReplyDeleteHere is my website - attorney bankruptcy lawyer
Here is my web page foreclosure law
Can Frd defeat Automobile
ReplyDeleteFeel free to visit my site :: attorney leads
Review my blog : lawyer search engine optimization