ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 6, 2012

TANZIA

 Kifo cha askofu ALOYSIUS BALINA wa jimbo katoliki la shinyanga kilichotokea leo siku ya jumanne majira ya saa tano za asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza alikokuwa amelazwa kwa matibabu na kimethibitishwa pia na Mkurugenzi wa habari wa jimbo kuu la Mwanza padre CHRISTOPHER KUBEJA pamoja na tanzia ya jopo la mapadri washauri wa jimbo la shinyanga.




Padri KUBEJA amesema kuwa mipango ya mazishi inafanyika jimboni shinyanga na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu... Msikilize kwa kubofya Play


TANZIA 
JOPO LA WASHAURI WA ASKOFU JIMBO KATOLIKI SHINYANGA KWA NIABA YA MAPADRE, WATAWA, WALEI NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA.

WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MHASHAMU ASKOFU ALOISIUS BALINA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA KILICHOTOKEA LEO TARAHE 6 NOVEMBER 2012 SAA 5:00 ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO.

HABARI ZIWAFIKIE MAASKOFU, MAPADRE, WATAWA NA WAUMINI WOTE POPOTE WALIPO.

MIPANGO YA MAZISHI INAANDALIWA JIMBONI SHINYANGA.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

IMETOLEWA NA 
MKURUGENZI WA HABARI 
JIMBO KUU LA MWANZA 
PADRE CHRISTOPHER KUBEJA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.