ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 2, 2012

UZINDUZI WA HEWANI WA TAMASHA LA "MTIKISIKO" 2012

Shangwe za ze Inshu....


Eddo Bashir (Mratibu Mkuu)

The Launching Continues na Promotions Manager (Bonny Zacharia Nyatogo)

Dj Alikoko (Entertainment Manager)

Dj Mubba

Host wa Show..Mkazuzu

           ON AIR
          Radio Ebony FM yenye makao yake makuu mkoani Iringa na inayorusha matangazo yake katika  masafa ya 87.8 (Iringa), 88.2 (Makambako), 94.7 (Mbeya), 91.6 (Dodoma), 95.4 (Morogoro) na 102.2 (Songea) jana Oct 01 kupitia kipindi chake cha mchana "THE SPLASH" imezindua hewani (on air launching) TAMASHA lake kubwa la kila mwaka maarufu kwa jina la "MTIKISIKO" ambalo linatarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu na kupita karibu sehemu zote inaposikika redio hiyo.

          Akizungumza katika uzinduzi huo Promotions Manager wa EBONY FM Bonny Zacharia Nyatogo amesema, mwaka huu EBONY FM ikishirikiana na kampuni mama ya burudani EBONY ENTERTAINMENT wamejipanga vya kutosha kukata kiu ya burudani kwa wapenda burudani wote kwenye mikoa ya Nyanda Za Juu Kusini ambayo wana uhakika haijakatwa bado.

          Mratibu mkuu ni Eddo Bashir kama ilivyo kwa miaka iliyopita, naye amesema maandilizi ya TAMASHA hilo yameshaanza na muda wowote kuanzia sasa ratiba rasmi itatangazwa hasa tarehe na maeneo TAMASHA hilo litakapopita. Kauli mbiu ya TAMASHA hilo mwaka huu ni "Ndo Vileee..!!!"

          Tamasha la "MTIKISIKO" kihistoria lilianza mwaka 2007 wakati huo likiitwa "PAMOJA TIME" ambapo mwaka 2008 lilibadilishwa jina na kuanza rasmi kuitwa "MTIKISIKO"...nia na madhumuni ya TAMASHA la "MTIKISIKO" ni kukutana pamoja na wasikilizaji wa ukweli wa EBONY FM na kurudisha kwao LOVE wanayotoa kwa redio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.