OCTOBA 11, 2012
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Chama Cha
ngumi za Kulipwa cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimetoa kibali kwa
promota Selemani Seminyo cha kuandaa pambano la kugombea ubingwa wa wa Afrika
ya mashariki na Kati katika uzito wa kati (middleweight) baina ya bondia Thomas
Mashali wa Tanzania na Sebayala Med wa Uganda.
Pambano hilo
litafanyika katika ukukumbi wa Friends Corner, Manzese, jijini Dar-Es-Salaam,
siku ya Jumapili tarehe 14 October, 2012.
ECAPBA
inajivunia kuwawezesha mabondia wengi kutoka katika nchi wanachama kuendeleza
vipaji vyao kwa kugombea mikanda ya ubingwa wake.
Tanzania ina
bahati ya kufanya mapambano mengi ya ubingwa wa ECAPBA na tunao mabondia wengi
ambao ni mabingwa ikilinganishwa na nchi nyingine.
Nchi wanachana
wa ECAPBA ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Ethiopia,
Sundan ya Kusini, DRC Congo na Zambia.
ECAPBA ilipendekezwa
kuundwa mwaka 2004 baada ya kikao cha kwanza nchini Kampala Uganda katika
hoteli ya Ghana kikiwashirikisha viongozi toka Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia na
Malawi na kufuatiwa na kikao cha uanzilishi mwaka 2004 katika hoteli ya
Kilimanjaro Crane mjini Moshi, Tanzania.
ECAPBA
inawaalika mapromota wengi kuandaa mapambano ya ubingwa kwa mabondia wengi
kwani hii ji njia mojawapo ya kuinua viwango vya mabondai wetu.
Aidha,
ECAPBA inawaomba wadau wa ngumi ikiwa ni pamoja na watu binafsi, makampuni,
taasisi za serikali na binafsi zijitokeze kwa wingi kudhamini mapambano yake ya
ubingwa kama njia mojawapo ya kuinua biashara zao na kuendeleza vipaji vya
mabondia nchini!
Shirikisho
la Ngumi la Afrika ya Mashariki na Kati limesajiliwa nchini Tanzania ambako
ndipo palipo na makao yake makuu kwa
sasa.
Viongozi wakuu
wa ECAPBA ni:
Rais: Onesmo
Alfred McBride Ngowi, TANZANIA
Makamu wa Kwanza wa Rais: Celestino
Mindra, UGANDA
Makamu wa Pili wa Rais: George
Uthman, KENYA
Katibu Mkuu: Shaaban
Ogolla, KENYA,
Mweka Hazina: Nemes
Kavishe, TANZANIA
Afisa Uhusiano: Paul
Chiwa, UGANDA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.