ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 8, 2012

MSANII LADY LUU HATUKO NAYE TENA

Huyu ndiye marehemu Lady Luu ayetutoka juzi na kuzikwa jana. 1977 -  2O12,  ameacha mume na watoto wawili.

Kwa kuwa CEO wa blogu hii yuko mapumzikoni (nje ya kanda ya ziwa). Twaomba radhi kwa kuchelewesha kuwafikishia taarifa hii. Ni taarifa ya kusikitisha kwa wana Mwanza na watanzania wote kwa ujumla, aliyekuwa maarufu msanii wa kwanza wa kike ambaye alihusika vyema ktk kundi la wateule aliye fahamika kwa jina la Lady Luu ametutoka.

Ilikuwa siku ya ijumaa na amezikwa ktk makaburi ya kitangiri jijini Mwanza.

Marehemu ata kumbukwa kwa kazi zake kama vile 'Haki hizo' na 'Hip hop na ragga' aliyo fanya na kundi la Wateule.
Apumzike kwa amani Lady Luu(luvina)

Ni mtoto wa pili na wa mwisho wa marehemu Lady Luu anae fahamika kwa jina la Pako Paul akiwa na mdau Philbert Kabago wa Passion Fm Mwanza pindi alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo aliyetutangulia mbele za haki

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.