Story
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewahimiza watanzania kuendelea kuchangia katika mradi wa kuchangia vifaa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum unaoendeshwa na Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (Bamvita)
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake, AY imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. Airtel inaamini kwamba watoto hao wenye mahitaji maalum wakiwezeshwa kielimu wataweza kutimiza ndoto zao na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi nchini.
Akiongea wakati walipotembelea shuleni hapo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema ” Ni matumaini yetu kuwa watanzania na wale wasio watanzania kwa ujumla wataendelea kutuunga mkono ili kuweza kutimiza lengo hili la awali na kisha kuongeza shule za mikoani mara baada ya kukamilisha mahitaji haya katika shule hizi za Dar es Salaam.
Kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na watanzania wanaweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na utakuwa umechangia shilingi 200 katika mradi huu au kupitia Airtel Money unapiga *150*60# ingiza jina la biashara VITABU na kuchangia kiwango chochote kile. Tunachukua fulsa hii kuwaomba watanzania wote kuchangia ili kuwafikia watoto wengi zaidi nchin”
Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya amesema “shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia. bila vifaa hivyo maalum itakuwa vigumu kwa wanafunzi kutimiza ndoto zao zakuendelea kielimu”.
Aidha Ameishukuru Airtel na BAMVITA kwa kuweza kuanzisha mradi huu na kuweza kuwahamasisha watanzania kuchangia ili waweze kupata vitendea kazi na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine.
Zena Yahaya Mwanafunzi Uhuru Mchanganyiko alikuwa na haya ya kuongeza “tunawashukuru Airtel kwa kuja kututembelea leo, tunawaomba watanzania wote waendelee kutusaidia kwa kushirikiana na Airtel katika mradi huu wa Vitabu ili kuweza kutusaidia katika kununua vifaa vya kutusaidia hapa shuleni na kuhakikisha tunapata elimu bora.”
Airtel inatambua umuhimu wa Elimu na tunaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe hivyo basi lengo la mradi huu ni kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza kuchangia elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwanunulia vitabu na nyenzo za walimu kufundishia. Kwa kuanzia tumeanza kutembelea shule mbili za jijinini Dar es Salaam zitafaidika na mpango huu ambazo ni Sinza Maalum, Uhuru Mchanganyiko ikifuatiwa na Buguruni Viziwi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.