HABARI
Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' 'amesema kuwa tuna muhandaa 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake huo
Tunamuhandaa vizuri ili aje kuwa bondia bora wa masumbwi hapa nchini unajua kuna stail nyingi sana za mazoezi ambazo anapewa ili kumkabili mpinzani wake kwa kuwa tunamjua vilivyo
Super D aliongeza kwa kusema kuwa mazoezi anayofanyishwa 'King Class Mawe' kwa sasa akuna mtu anaeweza kumfikia kwa kuwa kashavuka viwango bondia huyo anaecheza katika uzito wa Kg 60 amekuwa tishio kwa mabondia wezake baada ya mchezo wake wa mwisho kumdunda SakoMwaisege kwa K,O raundi ya tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, Dar-Es-Salaam
Na ataendeleza kupiga wapinzani wake kwa K,O katika raundi za mwanzo bila kuwachosha majaji pamoja na refarii wake
Aliongeza kwa Super D kuwa wanamfanyisha mazoezi ya kupiga kwa K,O ili aweze kuendeleza rekodi aliyonayo kwa sasa kwani mapambano yako yote matatu aliyocheza kapiga wapinzani wake wa K,O
| ||
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.