Ndugu, Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, amekipa usajili wa muda chama kipya cha siasa kinachojulikana kwa jina la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).
Chama hiki kinasimamiwa na mwanaharakati (utawala bora) maarufu nchini, Ndugu Walace Mayunga ambaye wenye chama wamemkabidhi kazi ya kukisajili hadi kipate usajili wa kudumu.
Makao Makuu ya CHAUMA ni Kijitonyama Mtaa wa Kameruni. Bandera ya CHAUMA ina rangi nne; nyeusi, nyeupe, nyekundu na njano. Kauli mbiu ya CHAUMA ni Nguvu ya Mabadiliko.
CHAUMA kinaonekana kuwa na mkakati mkubwa kwa sababu kinatumia waliokuwa makada wa CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP kutafuta wanachama 200 kutoka angalao mikoa 10 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa No. 5 ya 1992.
-Chanzo Mdau wa CHAUMA.
My take:Ni wazi kuwa mwenendo (kujitenga na M4C) na kauli za ZZK ambazo kila mara zinaonekana kuwa na malengo yaliyofichika; kujijenga binafsi (kupata wafuasi wengi) tayari kwa safari ya CHAUMA mara baada ya zoezi la usajili wa kudumu kukamilika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.