Mrembo Pendo Simon, (katikati) ndiye aliyetwa taji la Redds Miss Mwanza 2012/13, |
Dance la wanyange miss Mwanza. |
Smile |
Funguka |
Look |
Afro |
Yep.. |
Cat.. |
Parade.. |
We |
From wa last year to wa this year.. |
Mrembo Pendo Simon,ndiye aliyeshika taji la Redds Miss Mwanza
2012/13, ambapo aliwabwaga warembo 13 waliojitokeza kuwania taji hilo.
Shindano
hilo lilifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita katika viwanja vya Yatch Club
Mwanza, ambapo mgeni Rasmi alikua ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka
Konisaga.
Shindano lilianza kwa burudani ya warembo kutoa
show ya pamoja, ikifuatiwa na vazi la Ubunifu, Vazi la Ufukweni na
Mwisho Vazi la Usiku la kutokea. Warembo hao pia walipata fursa ya kuonyesha Vipaji vya aina mbalimbali.
Warembo
waliongia Tano Bora na baadaye kuulizwa maswali ni pamoja na Happiness
Daniel, Stella Augustino, Aisha Eddy, Clara Nuru na Pendo Simon.
Katika shindano hilo zawadi zilitolewa kama ifuatavyo
Mshindi wa Kwanza- 500,000/= na TV Inch
24
Mshindi wa Pili- 300,000/= na Decoder
Mshindi wa Tatu- 200,000/= na Decoder
Mshindi wa Nne- 100,000/=
Mshindi wa Tano- 100,000/=
Mshindi wa 6-13- 50,000/=
Wasani
waliopanda jukwaani kutumbiza ni pamoja na Mwanahawa Ally katika
miondoko ya Taarab, Bob Haisa na Jeeta Man kutoka Mwanza. Mwanamuziki
Khadija kopa hakuonekana kwenye jukwaa na kuwaacha mashabiki vinywa
wazi, ambapo alitangazwa kwamba angekuwepo. Baada ya kumuhoji Muandaaji
wa shindano hilo, John Dotto juu ya kutokuwepo Khadija kopa, hata yeye
alishangaa kutokuonekana malkia huyo wa Taarab, ambapo Dotto alidai
tayari alishalipwa pesa yote ya Show Shilingi Milioni Moja. Dotto
amesema walijaribu kuwasiliana naye kwenye simu ambapo malkia huyo
alidai yuko njiani akitokea Kahama kuja Mwanza, tangu saa kumi na moja
jioni siku ya tukio, hadi ilipofika saa 5 usiku hawakumuona mtu yeyote.
Inasikitisha kwa Mwanamuziki mkubwa
kama huyo kuchukua pesa za watu halafu hatokei kwenye shughuli.
Hii haimaanishi kulidhalilisha shindano, hii inamaanisha kujidhalilisha yeye mwenyewe.
Tupe maoni yako
Ndo tabia za wabongo wakiwa maarufu,sasa huyu mama nae ameshusha umalkia wake
ReplyDelete