ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 28, 2012

ZOEZI LA SENSA MKOA WA MARA LAENDELEA VIZURI

Mratibu wa Sensa mkoa wa Mara Bw Ramadhan Mbega



MUSOMA         
Augustine Mgendi                                                 
ZOEZI la Sensa na Makazi mkoani Mara  linaendelea Vizuri mpaka sasa licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo tangu kuanza kwake hapo Siku ya Jumamosi usiku chini nzima.

Akiongelea juu ya mwenendo mzima wa zoezi hilo Mratibu wa Takwimu mkoani Mara Bw. Ramadhani Mbega alisema kuwa mpaka sasa taarifa alizozipata kutoka sehemu mbalimbali mkoani Mara zinaashiria zoezi hilo kwenda vizuri.

Alisema Matatizo madogo ambayo yalikuwepo kama vifaa,picha kwa makarani kama utambulisho yametatuliwa na hivyo zoezi zima kuendelea kama lilivyopangwa.

“Kulikuwa na matatizo madogo hasa vifaa,picha kwa makarani lakini kwa sasa hali hiyo imerekebishwa na wanaendelea na zoezi vizuri” alisema Mratibu huyo

Aidha katika maeneo ya Mbugani na Visiwani,Bw Mbega alisema kuwa zoezi hilo limeendelea Vizuri kutokana na maandalizi yaliyokuwe hapo awali na wananchi wa maeneo hayo kuhamasishwa na kupewa elimu ya kutosha juu ya zoezi la Sense na Makazi

Mbali na maeneo hao Bw. Mbega alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo ambapo viongozi wa vijiji na vitongoji walikuwa wanalalamika juu ya maalipo yao na kuongeza kuwa malipo hayo yanatolewa kwa awamu kama ilivyoagizwa
Kwa sababu hiyo Mratibu huyo wa Takwimu mkoa wa Mara aliwataka wananchi wote wa Mkoa wa Maraa kuendelea kujitokeza katika zoezi hilo kwani kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali katika kupango mipango ya Maendeleo kwa wananchi.

‘Ya kikubwa mimi naomba wananchi waendelee kujitokeza katika seku zilizosalia ili tukamilishe zoezi hili vizuri kabisa kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia miapango ya Maendeleo kwa nchi yetu” aliongeza Bw Mbega
Mbali na kauli hiyo ya Mratibu wa Takwimu mkoani Mara Bw Ramadhani Mbega,baadhi ya wananchi ambao wamepata nafasi ya kuongelea zoezi hilo walisema kuwa mwenendo mzima wa zoeiz la Sense zi mbaya ingawa kuna baadhi ya Maeneo uelemishaji unaonekana kuwa mdogo
Mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tuppa
“Mimi naona zoezi linaenda vizuri ingawa kuna baadhi ya maeneo hali si nzuri sana kutokana na hamasa kuwa ndogo maeneo hayo” Alisema Juma Omary mkazi wa Kamnyonge mjini Musoma
Hivi karibu akizindua zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. John Gabriel Tuppa ambaye pia ni Mwenyekiti wa katika ya zoezi hilo mkoa wa Mara alisema kuwa zoezi hilo halipaswi kuunganishwa na masuala ya dini kwani lengo la Serikali siyo kujua idadi ya waumini hapa nchini.
Alisema ni vyema watu wakaliunga mkono zoezi hili kwa asilimia kubwa ili Serikali katika mipango yake iweze kufanikisha kufikisha Maendeleo kwa Wananchi

www.mwanawaafrika.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.