Wednesday, August 08, 2012
|
Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani |
|
Nakala ya barua inaendelea hapa |
|
Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande Dunga. |
Na.Danstan Shekidele
Siku
chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald
Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani
Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza
kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini,
imebainika.
Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga
aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa
kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa
dhidi ya maofisa hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine
Shilogile, jana (juzi) alisema jeshi hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga
Mathew jana (juzi) asubuhi.
Alisema askari huyo, aijinyonga kwa kutumia
vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na hakuacha ujumbe
wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.
Inatajwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo, askari huyo alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.
Alisema
baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki
mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo,
kumfuata na kumsihi avae nguo.
Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi. “Pamoja
na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado
tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili
wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,”
alisema Kamanda Shilogile.
Alipoulizwa kama kifo cha Mathew
kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za
kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema
uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna askari aliyehusika
atachukuliwa hatua kali.
Hata hivyo, askari huyo mwishoni mwa
mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika moja ya
magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa
kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa
kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Tuhuma nyingine
alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa
baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha
kituoni.
Alisema tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata
wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia
hatua zozote baada ya kuhongwa.
Tuhuma nyingine, zinazodaiwa
kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia wa
kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za
wafanyabiashara nyakati za usiku.
Chanzo/Blogzamikoa
www.blogszamikoa.blogspot.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.