Wednesday, August 08, 2012
|
Mtuhumiwa wa kudurufu kazi za wasanii akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa. |
|
Msanii MOHAMED
'NICE' akilia kwa uchungu baada ya kukuta kazi zake zikiuzwa bila ridhaa yake kwenye moja ya duka mtaa wa Magila na likoma jijini Dar. |
|
Msanii
wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB'
wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki
ambapo walikamatwa kwa kushilikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps
Entantainment ya jijini Dar es salaam |
|
Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi za wasanii
mbalimbali nchini zinazouzwa kiholera baada ya kurudufu kinyume na
sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri. |
|
Baadhi ya watu wakiwa wamezagaa kushuhudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma Dar es salaam |
|
Baadhi ya kazi feki zilizokamatwa. |
|
Wananchi mashuhuda. |
|
|
|
|
Msanii Kapten Rado akikagua kazi zake mpya ambayo inajulikana kama 'HATIHANI' iliyoingia mtaani leo ikiwa tayari imekwisha chakachuliwa na kuingizwa sokoni. |
|
Kazi za Mzee Yusufu nazo zipo nyingi tu ambazo nifeki.... |
TAARIFA KAMILI
KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar
es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii
wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na
taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo
Msemaji wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa
ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii
wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao
zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa
tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili
iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo
Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo
iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii
Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani
katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na DVD ndio inakuwa
imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa
masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao
bila kushiriki chochote
Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja
na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni
Mwapagata (
Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles
Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana
pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na
kuiomba serekali kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama
hizo zilizokamatwa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.