ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 8, 2012

TAMASHA LA SIMBA DAY LATIBUKA,YACHAPWA 3-1 NA NAIROBI CITY STARS UWANJA WA TAIFA JIONI HII

Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Nairobi City Stars katika mchezo wa kirafiki wa tamasha la Simba Day linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tamasha hilo limeandaliwa na klabu ya Simba na hufanyika  kila mwaka Agosti 8 na kushirikisha timu marafiki wa klabu hiyo huku wachezaji na viongozi mbalimbali wakipewa zawadi kwa mchango wao kwa klabu hiyo, Katika mchezo wa leo, hivi sasa mpira umekwisha na Simba imefungwa magoli 3-1 na timu  ya Nairobi City Stars kutoka nchini Kenya

Hili ndilo benchi la ufundi la timu ya Nairobi  City Stars kutoka nchini Kenya
Benchi la ufundi la timu ya Simba kushoto ni kocha wa timu hiyo Bw. Milovan.
 
Kikosi cha timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa paambano hilo.
 
Kikosi cha timu ya Nairobi City Stars kutoka Kenya kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa paambano hilo.
CHANZO FULL SHANGWE BLOG

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.