ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 8, 2012

NI SIKUKUU YA 88 MWANZA NDANI YA NYAMONGOLO GROUND

Ni maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nchini Tanzania al-maarufu kwa jinala Sikukuu ya Nane nane hapa makarai, vikaangio, miko, majiko na baadhi ya pembejeo za jikoni zikiuzwa katika viwanja vya Nyamongolo, Igoma jijini Mwanza.

Wadau wa mataifa ya mbali nao wamezipenda bidhaa hizi.

Dakitari wa dawa zitokanazo na mitishamba Dr. Hoze amesafiri kutoka Uyole jijini Mbeya kwaajili ya kutoa huduma ya dawa asilia maonyesho jijini Mwanza hapa akizungumza na mteja wake.

Ni kitalu cha maonyesho mbegu bora za dengu ambazo ziko aina kwa aina.

Zao la 'ubwechee' (Mpunga) nalo lilikuwa na somo lake kwenye maonyesho haya.

Ni shamba lisilo tumia mbolea za kemikali ambazo zina madhara makubwa kwa udongo na viumbe hai asilia waishio kwenye udongo, mbolea izalishwayo kutoka mimea aina ya ndulele inamanufaa na kinga kwa udongo, ni elimu tosha ukifika banda hili la kilimo na kujionea mwenyewe.

Mkurugenzi wa Kahama Lishe Product Eva W. Nnko akimwonjesha ladha ya moja ya bidhaa zizalishwazo na kampuni yake mteja wake, bidhaa zinazosindikwa na kampuni hiyo ni kama Tangawizi, Viungo vya pilau, Pilipili manga, Mdalasini, Kahawa, Chai n.k.

Wateja wakijichukulia vyao ndani ya banda la Kahama Lishe Product.

Wakulima wengi miaka ya sasa wamebobea kuzithamini mbolea za kemikali ambazo zinamadhara makubwa kwa afya ya ardhi, mazao na walaji hapa somola mbolea asili lilikuwa likitolewa.

Banda la Mwanza Quality Wines watengenezaji wa mvinyo saaaaaaafi....

Mambo ya ujenzi...

Tembea uone....siyo maghorofa bali....

Banda linalojihusisha na uzalishaji mbegu za mazao la Quton ambalo lilikuwa kivutio kikubwa kwa wakulima wengi waliofika viwanja vya Nyamongolo jijini Mwanza kushuhudia maonyesho ya 88 mwaka 2012.

Mkulima akipata maelezo juu ya mbegu...

'Sasa ni wakati wa kuvuta pumzi' ni kama vile Bi Irene Makene akisemezana na mdau mwenzake ndani ya banda la ushauri na uzalishaji na uuzaji mbegu la Quton mara baada ya kuhudumia wateja waliofurikakwa wingi kwenye banda lao hadi tamati. Quiton ni Banda ambalo limekuwa moja kati ya mabanda yaliyotoa mchango mkubwa kuongezea ujuzi wakulima kwa maonyesho haya ya mwaka 2012 mkoani Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.