Josee Mara amesema wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna wanamuziki wengine kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama ilivyokuwa kwa Kalala Jr. "Na sasa hivi nakuhakikishia Da'Suzzy tutapiga kazi ile mbaya, kwa sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki wazuri na tunawahamu toka kitambo, kwa hivyo naamini mambo yatakuwa sawa na washabiki wetu wasivunjike moyo, waendelee kutuunga mkono tu, sisi ni wapambanaji kwa hiyo ni lazima tupambane"amesema Josee Mara.
Aidha Khalid Chokoraa ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti wamekwisha rekodi singo yao moja iitwayo ONA NAONEWA,ambayo wataitambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wa muziki wa dansi
Mmoja wa watangazaji
wa Clouds FM,kupitia kipindi cha Wikend Bonanza,Da' Suzzy akizungumza na
wanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini waliokuwa wakijiita Mapacha 3, ambapo kwa
sasa mmoja wao Kalala Jr ameamua kuachia ngazi na kuwaacha wenzake Khalid
Chokoraa na Josee Mara kama uwaonavyo pichani wakiwa na Meneja wao Hamis Dacota
pichani kulia.
Da'Suzzy alikuwa akitaka kujua kwanini msanii mwenzao Kalala Jr
ameamua kutimka kwenye bendi yao na kwamba wana mikakati gani ya kuliziba pengo
la mwanamuziki huyo aliyetimka.Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo ya Mapacha
3, Hamis Dacota amebainisha kuwa Kalala Jr aliamua kuondoka mwenyewe bila kuwepo
na ugomvi wowote baina yao, "hivyo kama mwanamuziki mwenzetu,kijana mwenzetu
tunamtakia kila kheri huko aendako,lakini kama akitaka kurudi pia milango iko
wazi anakaribishwa sana, kwa sababu yeye ni mmoja wa waasisi wa bendi ya mapacha
3", alisema Dacota.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.