■ Deidre Lorenz kukisaidia kituo cha watoto
yatima cha Upendo cha Moshi
Balozi wa
Heshima wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon katika jiji la mapesa la New York
City (NYC) nchini Marekani ambaye pia ni mcheza sinema na mlimbwende maarufu
kutoka jiji hilo linaloaminiwa kuwa kitovu cha pesa duniani, Mmarekani Deidre
Lorenz ameahidi kukisadia kituo cha watoto yatima cha Upendo kilichopo katika
Manispaa ya Moshi.
Lorenz
alikitembelea kituo hicho siku mbili (tarehe 22 Juni) kabla ya kukimbia mbio za
Mt. Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 juni mwaka huu kuanzia
Moshi Club hadi Rau mudukani.
Mbio za Mt.
Kilimanjaro Marathoni zilianzishwa na Marie Frances anayetoka katika jiji la
matajiri la Bethesda nje kidogo ya jiji la Washingyon DC nchini Marekani mwaka
1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani nchini Misri.
Marie
Frances aliyekuwa muandaaji wa vipindi vya television ya ABC alianzisha mbio za
Pyramid Marathon zilizofana sana nchini Misri na kumfanya balozi wa Tanzania
nchini Misri wakati ule kumuomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon.
Mt.
Kilimanjaro Marathon ilianzishwa mwaka 1991 katika Manispaa ya Moshi zikiwa ni
mbio kukimbia kwa furaha (fun run) inayowaleta wazungu kupanda mlima
Kilimanjaro, kukimbia na kwenda kutembelea mbuga zetu za wanyama. Mbio hizi zipo
katika kiundi la Seven Continental Marathons ambazo hukimbiwa katika mabara saba
ya dunia.
Deidre
Lorenz ambaye amewahi kuigiza katika filamu nyingi alipatikana katika bahati
nasibu (Raffle) iliyochezeshwa na Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 wakati wa mbio
za New York Marathon jijini New York Marekani mwaka 2011. Katika bahati nasibu
hiyo Deidre Lorenz aliibuka mshindi na kujipatia tiketi ya bure pamoja na
gharama za hoteli za kuja kukimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon mwaka
huu.
Wadhamini wa
mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon ni kampuni ya ndege ya Ethiopia Airlines (ET)
ambayo huwa inantoa tiketi za bei rahisi kwa wale wanaokuja kukimbia mbio hizo.
ET pia hugharamia ushiriki wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 katika mbio za New
York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Marathon ili kijitangaza.
Katika
mpango huo Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 huweka banda la kutangaza vivutio vya
Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, Zanzibar na mali zetu za
asili.
Mkakati huu
umesaidia sana kuitangaza Tanzania na hivyo kuwapa fursa watalii wengi kutoka
Marekani na nchi nyingi duniani kuijua vyema Tanzania. Wengi wa wakimbiaji hawa
hutembelea vivutio vya Tanzania baada ya kutembelea banda la Mt. Kilimanjaro
Marathon 1991 katika mbio hizo.
Ufadhili wa
Deidre Lorenz akishirikiana na taasisi ya Screen Actors Guild utakisaidia sana
kituo cha watoto yatima cha Upendo ambacho kinakabiliwa na changamoto nyingi za
fedha na vifaa vya kuwatunza watoto wanaolelewa kituoni hapo. Kituo hiki
kilianzishwa miaka ya 60 na masista wa shirika la Precious Blood wa Kanisa
Katoliki jimbo la Moshi.
Kwa miaka
mingi kituo hiki kimekuwa kinapokea watoto wachanga wanaotelekezwa na mama zao
baada ya kuzaliwa katika hospitali mbalimbali za mkoa wa Kilimanjaro. Kituo cha
Upendo kinawapokea pia watoito ambao mama zao wamefariki wakati wa
kujifungua.
Aidha Lorenz
ameahidi kuwashawishi walimbwende na wacheza filamu wengine wa Marekani kuja
kushiriki katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na kutembelea vivutio vya
kitalii vya nchi hii kila mwaka.
Imetumwa na
:
Grace
Soka
Afisa Uhusiano
Afisa Uhusiano
Mt.
Kilimanjaro Marathon 1991
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.