Tamko hilo limetolewa jana na Waziri wa mifugo na uvuvi Mathayo David Mathayo wakati alipokutana na wavuvi, wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki katika kikao cha kujadili mgogoro uliosababisha wavuvi kugoma na viwanda kutetereka kiuzalishaji.
Kuhusu mgogoro uliodumu takribani mwezi mmoja sasa Waziri David Mathayo, akiwa ameambatana na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo, amewashauri wavuvi kuanzisha ushirika wa pamoja utakao wasaidia kutambua bei halali, kudhibiti bei duni na mapungufu yasiyo ya lazima yanayojitokeza.
Katika maazimio Kamati hiyo ya bunge imeshauri kuwepo kwa mikataba ya aina moja baina ya wavuvi na wamiliki ambayo itapitiwa na wanasheria wa pande zote mbili chini ya usimamizi wa serikali wakati wa kuandaliwa hatimaye utekelezwaji ili kuepuka migogoro ambayo ni chanzo cha migogoro kupitia dhuruma inayopelekea kuporomoka kwa pato la Taifa.
Mjumbe wa kamati mh. Moshi Selemani Kakoso (Mbunge wa mpanda vijijini) akitoa maelezo ili kupata ufafanuzi. |
Licha ya kamati hiyo kuwasihi wamiliki wa viwanda kupandisha bei ili kukidhi gharama za mvuvi lakini kutokana na sababu walizoambatanisha wakakomea hapo.
Wavuvi kikaoni. |
Mjumbe wa kamati hiyo toka bungeni mh. Dr. Titus Kamani (Mbunge wa Busega). |
Wakurugenzi wa viwanda mbalimbali Mwanza. |
Meza kuu mkutanoni kutoka kushoto ni wajumbe wa kamati ya kilimo na mifugo Rose Kamili (Mbunge wa viti maalum CHADEMA - Manyara) na mh. Dr. Titus Kamani (Mbunge wa Busega) wakiwa na Waziri wa mifugo na uvuvi mh. Mathayo David.
Suala lingine walilolalamikia wavuvi ni kwamba samaki anapo fikishwa kiwandani na kutajwa kuwa ni reject harudishwi na kiwanda hivyo kamati hiyo imetamka kuwa kama samaki ni reject basi arudishwe kwa mvuvi badala ya viwanda kuchukuwa reject hao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.