Nahodha wa timu ya wasichana ya mkoa wa Mbeya Mariam Ndauka, akinyanyua juu kombe baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars kwa wanawake baada ya kuifunga Arusha 1-0 kwenye fainali za Airtel Rising Stars zilizofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa timu ya wavulana ya Temeke Khalid Salum, akipokea kikombe kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michez,o Juliana Matagi Yasoda. Temeke iliibuka mshindi wa michuano hiyo kwa wanaume baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Karume Jumapili 17 jijini Dar es Salaam.
Time ya Temeke ikifurahia ushindi mara baada ya kuibuka kuwa washindi wa michuano ya Airtel Rising Stars kwa kutwaa ushindi wa mabao 3-1 thidi ya timu ya Mbeya
Wachezaji nyota 6 wa michuano ya Airtel Rising stars wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa jana katika michuano ya Finali iliyofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.
Temeke, Mbeya mabingwa michuano ya
ARS
Fainali za taifa michuano ya
Airtel Rising Stars iliyokuwa ikihusisha timu za mpira wa miguu kwa timu za
wavulana na wasichana, zilifikia tamati Jumapili 17 kwenye Uwanja wa Karume huku
timu za wavulana Temeke na Mbeya wasichana zikiibuka mabingwa wa michuano
hiyo.
Michuano hiyo ya vijana wenye
umri chini ya miaka 17 pia imetoa wachezaji sita bora ambao watahudhuria kliniki
ya soka ya Kimataifa itakayokuwa chini ya walimu kutoka Klabu ya Manchester
United ambayo itafanyika Nairobi. Wachezaji hao ni – Jackline Gibson na Irene
Bahisi kutoka Arusha, Madeline Sylvester (Ilala), Abdul Seleman, Denis Richard
na Paul Balama (Temeke).
Jumla ya timu za shule za
sekondari 24 kutoka mikoa sita zilishiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa
mwaka huu huku wachezaji bora wakichanguliwa kuunda timu kombaini za mikoa kwa
ajili ya fainali za taifa. Mikoa iliyoshiriki ni Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala,
Kinondoni na Temeke.
Shule hizo zilichanguliwa
kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya taifa ya shule za sekondari
(UMISSETA) mwaka jana. Uzinduzi rasmi wa ARS 2012 ulifanyika Mei, kwenye Hoteli
ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester
United ya Uingereza, Quinton Fortune.
Fainali za ARS za wiki moja pia
zimetumika kuchangua timu ambayo itawakilisha Tanzania kwenye michuano ya
‘inter-continental’ ambayo itashirikisha nchi 17 ambao Airtel inafanya biashara.
Michuano hii itafanyika Nairobi mwezi wa Agosti.
Timu ya wavulana ya Temeke
imepata nafasi ya kuwa bingwa wa Airtel Rising Stars 2012 baada ya kuifunga
Mbeya 3-1 kwenye fainali kali y a kusisimua huku wasichana wa Mbeya wakiibuka
bingwa baada ya kuwafunga wenzao Arusha 3-1. Timu hizo mbili bingwa
zilijinyakulia vitabu vya thamani ya Tshs1m, medali ya dhahabu na vyeti vya
kushiriki.
Michuano wa Airtel Rising Stars
ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya
soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye miaka chini ya kumi na saba
ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira
wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji
vyao.
Airtel Rising Stars ni ushirikiano kati ya Airtel na klabu ya Uingereza
ya Manchester United ya kukuza vipaji vya soka barani Afrika. Huu ni mwaka wa
pili kwa Airtel kudhamini michuano hii. Mwaka jana, Klabu ya Manchester United
ilitoa walimu wake wa soka ya vijana kuendesha kliniki ya soka ya Kimataifa
ambazo kliniki hizo zilifanyika Tanzania, Afrika Kusini na Gabon.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.