ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 19, 2012

MNYIKA ANGEKUWA DHAIFU ZAIDI KAMA ANGEFUTA KAULI YAKE BUNGENI.


Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea. Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu.

MNYIKA ANGEKUWA DHAIFU ZAIDI KAMA ANGEFUTA KAULI YAKE BUNGENI.
1. Kama udhaifu ni kuto kujua kwa nini wananchi wako ni maskini
wakati wako nchi tajiri. Mnyika yuko sahihi.

2. Kama huwezi kumuwajibisha au kuona madudu ya katibu mkuu au katibu
kiongozi mpaka bunge lishikilie bango na kushinikiza wang'oke ndio
uzinduke kufanya maamuzi basi mnyika yuko sahihi.

3. Kama kweli watu wamelibia taifa kupitia dili za magumashi halafu
una watangazia warejeshe fedha ili wasichukuliwe hatua na wakati
huohuo vibaka wanauwawa au kuchomwa moto kwa kuiba kuku na simu basi
ni dhahiri kuna udhaifu wa kiungozi. Mnyika yuko sahihi.

4. Kama ndege inaingia kwenye anga ya nchi yako na kubeba wanyama
kupeleka Arabuni bila hatua zozote kuchukuliwa ni dhahiri kuna udhaifu
wa kimfumo ulio kubuhu serikalini. Mnyika yuko sahihi.

5. Kama rais anafunga safari kwenda kuomba misaada na wakati huohuo
misaada anayopewa hailingani thamani na raslimali zinazo vunwa kwenye
nchi yake basi Mnyika yuko sahihi.

6. Kama rais anadiriki kutoa ahadi 99 ambazo thamani yake ni zaidi ya
trilion 9 huku akijua kuwa hazitekelezeki ni hadaa kwa wananchi, chama
na serikali. Mnyika yuko sahihi.

7. Kama taasisi ya Ikulu na mfumo wake wa utawala umehusika kuingilia
maamuzi ya mhimili wa haki kwa kutoa hukumu ya upendeleo ili kumkomoa
au kumnyang'anya mbunge wadhifa kama jinsi ilivyo lalamikiwa. Mnyika
yuko sahihi.

8. Kama serikali inatenga 70% kwa matumizi kwenye bajeti yake na 30%
kwenye maendeleo. Ni dhahiri kuwa ni aina ya serikali dhaifu yenye
viongozi wavivu wa kufikiri.

Kama hivyo ndivyo, nasimama na kijana mwenzangu kwa ukakamavu na
kupaza sauti yenye mwale mkali. Namuunga mkono Mnyika.


Mnyika amekisema kile kinachosemwa na baadhi ya wananchi wenye
ujasiri, tofauti yake na yetu ni kwamba yeye kasemea bungeni sisi
tunasemea vijiweni tukinywa kahawa.



Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Hatupendi tu "Black and white"..lakini majibu yapo wazi kabisa!!!!!!!
    Mashafi C.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa Rais wetu ana udhaifu, ni kutokana na urafiki anashindwa kukemea maovu ya watu wake wa karibu.

    Nchi hii wanaofaa kupewa nyadhifa ndio waodharauliwa na kufunikwa ili wasitokee kabisa ktk jamii. Hata kina Mnyika wana risk maisha yao sana kuongelea mambo yanayotungua macho ambayo waTZ wengi katika hali ya kawaida tusingeyajua. Hawa wamejitolea sana kwa niaba ya walala hoi wengi,nawapongeza sana. Fikiria bila CHADEMA ya sasa, watanzania tungethaminika hata kwa haya machache yanayoboreshwa kutokana na kelele zinazopigwa na watu kama kina Mnyika?

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.