Chungulia mahojiano na wachawi hao wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza katika video.
Nabii Abigaili Zumaridi wa kanisa hilo Ufunua akisimulia kilichotokea.
Watu hao wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa majira ya saa 12 asubuhi leo katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.
Kwa mujibu wa mahojiano waliyofanya na blogu hii wachawi hao wanasema kuwa walipewa amri na wakuu wao wanao ishi chini ya maji kuwachukuwa watu watatu wa kanisa hilo kwa mazingira ya kichawi ili wawauwe kwaajili ya kafara na mazindiko.
Pembejeo za kichawi mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.
Wananchi na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi Mwanza wakiwa wamewazingira wachawi hao katika viwanja vya polisi Mwanza leo asubuhi katika kuchukuwa maelezo.
Mchungaji wa kanisa la Ufunua Diana Bandele (kushoto) na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa hilo ambao waliwakuta wachawi hao kanisani mwao majira ya saa 12 kwani muda huo ni ada kwa wao kujitakasa kwaajili ya kuianza siku ya ibada.
Ingawa jeshi la polisi linaendelea kuchunguza juu ya hali hiyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna kipengele kinacho utambua uchawi hivyo hakuna kesi inayowakabili watu hao.
Tupe maoni yako
Hawana uchawi wowote, njaa tu ndio inawasumbua. Watafutieni kazi muone kama wataendelea kuhangaika usiku kucha.
ReplyDeleteUchawi upo lakini kwa njia hiyo ya wawili hao. Haikubaliani akil yangu inakataa. Kwanini wasiwachukue kabla ya kuingia kanisani?kwanini wasishike utawala ikiwa wana uwezo huo? No. No No .
ReplyDeletePropaganda za PR Marketing for the churches hakuna lolote
ReplyDeleteuchawi upo na kama hamuamini nenda buha
ReplyDeleteuone
Pr. anatafuta wateja wa sadaka
ReplyDelete