ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 21, 2012

JUHUDI ZA UNDER THE SAME SUN KATIKA KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA UONO HAFIFU KANDA YA ZIWA

Mwanzilishi wa Shirika la mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Under The Same Sun) Peter Ash akiwa amembeba mmoja kati ya watoto 23 waliofanya vizuri kwenye masomo na kutunukiwa medali katika shule ya Lake View jijini Mwanza.
Shirika hilo linalotoa udhamini wa elimu kwa watoto wapatao 64, kati ya hao 23 wamefanya vyema kwenye mitihani shule mbalimbali za msingi jijini Mwanza, huku watoto 17 wakishika nafasi ya 1,2,na 3 hali hiyo ikichangiwa na kuwawezesha watoto hao vifaa maalum vya kuweza kuona na kusoma bila shida (miwani na lensi maalum).
Watoto ndani ya chumba cha kuzawadiwa medali.
Aidha Shirikahilo limetoa semina kwa walimu wa shule zinazowalea watoto wenye ulemavu wa ngozi na uono hafifu za Lake View na Jeris zote za jijini Mwanza, elimu ya jinsi ya kuwatunza, kuwalea pamoja na kuwahudumia. 
Under The Same sun pia ilishiriki kugawa kofia na mafuta maalum ya ngozi kwaajili ya kujikinga na mionzi mikali ya jua pamoja na kuwapima macho na kuwafanyia utafiti watoto wenye uono hafifu. 
Mafuta maalum yaliyogawiwa kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya maradhi ya kansa ya ngozi.
Mtoto Maisha Msobi mwanafunzi wa 'prep one' akiniandikia jina lake huku mapacha wawili Matias na Yohana, macho wakiyaelekeza kwenye kamera yako.
Wakipata flash ya pamoja kutoka kushoto ni Heri Abel, Matias, Yohana na Maisha Msobi

Madam Jackline Raymond anasema 'Tuwatunze watoto wasicheze kwenye mionzi ya jua kali tofauti na jua la asubuhi ambalo ni muhimu kwani lina vitamini muhimu kwa ngozi" Vilevile mwalimu huyu ametoa wito kwa serikali kulibeba suala hili mgongoni kama ilivyoweza kulibeba suala la malaria na gonjwa la ukimwi katika mapambano.
"Naishukuru jamii ya watanzania inayoonekana kubadilika kwa kasi kifikra zamani sisi hatukupewa nafasi katika jamii zilizotuzunguka, tulitengwa kielimu hata pale tulipoonekana kufanya vizuri nafasi hatukupewa, lakini sasa jamii inashituka na kutupa majukumu" says Kondo Adui Seif, Advocacy and Public Awareness Under The Same Sun. 
Rais wa Under The Same Sun Peter Ash, kwa mara ya kwanza alitambulisha kwa watoto mchezo wa magongo (Hockey game) ambapo pamoja na kuwafundisha jinsi ya uchezaji pia alikabidhi vifaa vya uchezaji mchezo huo.

Fun ....Oh yeah....!!!!

Mchezo ukiwa umekolea bin kunoga, pale kati namwona rais wa Under The Same Sun (Peter Ash) na  mkurugenzi wa shirika hilo nchini dada Vick Mketema, wakijumuika mchezoni....

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.