Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akijiandaa kukabidhi kiasi cha fedha shilingimilioni 9 kwa uongozi wa timu ya Pamba ya jijini Mwanza ndani ya ofisi zake. |
Wito umetolewa kwa wakazi wa Mwanza na wadau wote wenye mapenzi ya maendeleo ya soka la kanda ya ziwa kushiriki kikamilifu kuchangia maendeleo ya soka mkoa wa Mwanza na wilaya zake.
Mkuu wa mkoa akikabidhi milioni 9 kwa mlezi wa timu ya soka ya Pamba Charles Masalakulangwa. |
Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo wakati akiikabidhi timu ya soka ya Pamba kiasi cha shilingi milioni 9 taslimu kwaajili ya maandalizi ya kujiandaa na michuano ya makundi kuwania nafasi kutinga ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
Pamba iliyopangwa katika kituo cha mkoa wa Kigoma inahitaji kuwa na kiasi cha shilingi milioni 25 ili kuweza kushiriki vyema mashindano hayo.
Uongozi wa timu ya Pamba kutoka kushoto ni Mlezi wa timu hiyo Charles Masalakulangwa, Omar Manjicha ambaye ni katibu wa timu na Kazimoto Muzo ambaye Mwenyekiti wa timu. |
Akipokea kiasi hicho cha fedha hizo taslimu milioni 9 mlezi wa timu ya Pamba Charles Masala Kulangwa ameahidi kukamilisha mpango ulioazimiwa kwani anaamini kikosi kilichopo kina ubora stahiki kutinga ligi kuu soka Tanzania bara.
Nacho chama cha soka mkoa wa Mwanza kupitia katibu mkuu wake Nasibu Mabrouk kimewaahidi wapenzi wa soka kuwa kamati yake itasimamia suala la matumizi ya fedha kwa nidhamu ya hali ya juu ili kufikia malengo tajwa.
Mkuu wa mkoa na wadau wa soka pamoja na waandishi wa habari. |
Blogu hii inatoa Shukurani kwa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Halmashauri ya jiji na Nyanza Road Works kwa kuonyesha mfano, ni matumaini kuwa itakuwa chachu kwa wadau wengine kusapoti maendeleo ya soka nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.