Toto ndiyo walikuwa wa kwanza kujipatia bao katika dakika ya 11 mfungaji akiwa ni Musa Said mara baada ya kupokea pande safi toka kwa Mohamed sudy na kuichambua vyema ngome ya Yanga hakuwa na sababu ya kutopasia nyavu.
Bao hilo liliamsha ari na nguvu kwa Toto huku wachezaji wake Musa Said, Emmanuel Sita na Sudy Mohamed wakionana vilivyo na ilikuwa Idd Moby katika dakika ya 26 ndiye aliyewanyanyua tena mashabiki wa Toto kwa kuipatia timu yake bao la pili.
Dakika 10 baadaye ilikuwa ni zamu ya Musa Said kufanya kweli tena kwa kuipatia Toto bao la 3.
Toto walionekana kurizika mara baada ya goli hilo hali iliyosababisha Yanga kuutumia mwanya huo kujipatia bao la kwanza kupitia Kiiza, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga 1, Toto 3.
kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kutandaza soka safi, mabadiliko yaliyofanyika upande wa Yanga kumwingiza Shamte Ali na kumtoa Rashid Gumbo vilevile Asamoah kuingia dimbani kuchukuwa nafasi ya Zuber Ubwa yaliiongezea kasi timu hiyo na ilikuwa ni dakika ya 16 Kiiza tena akaipatia Yanga bao la pili.
Hadi mwisho katika dimba la CCM Kirumba Mwanza mchezo wa ligi kuu Wanakishamapanda (Toto Africans) 3, Yanga 2.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.