Ameamua kuanzisha programu hiyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwa na pumzi na nguvu kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani.
Akizungumza leo, Kocha huyo alisema kuwa mabondia wake watashiriki katika mashindano ya 10 bora yaliyoandaliwa na Kinyogoli Foundation yatakayofanyika May 4.
Alisema kuwa mabondia hao watazichapa katika mpambano wa aina yake utakaofanyika mwezi ujao katika Ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.
“Nimeanzisha programu ya aina yake kwa ajili ya kuwajengea uwezo mabondia wangu ili waweze kuwa na pumzi za kutosha katika mashindano mbalimbali” alisema. Super D
Aidha aliongeza kwa kusema wanaomba wadhamini kujitokeza kusaidi vitu mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mchezo huo wa masumbwi kwa kuwapatia vijana maja ata zawadi ndogo ndogo za kuwatia moyo mashindano hayo yatakayowashirikisha vijana mbalimbali katika uzito tofauti yatakuwa na lengo la kuendeleza mchezo wa masumbwi Nchini
Mapambano yatakuwa mengi kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kuja kujiandikisha kushiriki siku hiyo alisema Super D
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.