ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 2, 2012

'NI NASARI NI CHADEMA ARUMERU MASHARIKI'

Kushoto ni Mkazi wa Arumeru Mkoani Arusha, akipiga kura katika kituo cha Ngaresero, uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi wa gazeti la Mwananchi.
Matokeo ya uchaguzi wa Ubunge wilayani Arumeru Mashariki yametangazwa rasmi asubuhi ya leo mara baada ya zoezi la kuhakiki uhesabu kura lililochukuwa muda mrefu kukamilika na matokeo yakimpa ushindi mgombea wa CHADEMA bwana Nasari Joshua;

KURA HALALI: 60038
ZILIZOKATALIWA: 661
Wagombea:
Mazengo Adam AFP 139

Charles Msuya UDP 18

TLP 18

Kirita Shauri Moyo 22

Hamisi Kiemi 35

Mohammed DP 77

Sumari Solomon CCM 26757

Nassari Joshua CHADEMA 32,972

Huu ni uchaguzi wa kwanza mdogo kwa CHADEMA kushinda katika jimbo lililokuwa likishikiliwa na CCM na uchaguzi wa pili kwa chama hicho cha upinzani, kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya ule uliofanyika katika Jimbo la Tarime, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Wow. Hongera wana- Chadema wote Tanzania na nje ya nchi.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.