Matokeo ya uchaguzi kiti cha udiwani yametangazwa rasmi jioni ya leo yakimpa ushindi mgombea udiwani kupitia tiketi ya CHADEMA Bahati Kahungu kwa tofauti ya kura 807 kwa mgombea aliyekuwa akichuana naye kwa kasi Jackson Robert 'Masamaki' wa CCM.
Vituo vyote vilimaliza majumuisho yake mapema hivyo zoezi lililokuwa limebakia hadi kufikia saa moja jioni ilikuwa ni kufanya majumuisho ya vituo vyote kisha matokeo yapate kutangazwa, yote yakijiri wafuasi wa CHADEMA walikuwa wakiimba huku wakizunguka viwanja vya Furahisha kusherehekea matokeo ya vituo vingine.
Jeshi la polisi lilijizatiti vilivyo katika suala la ulinzi.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe aliwasili viwanjani hapo kutuliza wafuasi wa chama hicho kujiepusha na vurugu kwani haki imezingatiwa.
Zito Kabwe ilimbidi kutumia kipaza sauti kuhamasisha utulivu kwani kulikuwa na kila dalili za machafuko kutokea kwa kila mmoja kuwa na imani yake dakika chache baadaye matokeo yalitangazwa na Afisa mtendaji wa kata ya Kirumba Aloyce Mkono: CHADEMA kura 2938 CCM kura 2131 CUF kura 184 UDP kura 7 NCCR kura 0 Mara baada ya matokeo hayo kutangazwa hali ya utulivu ilitawala watu wakiamuriwa kuondoka kwenye eneo hilo.
Askari akiamuru watu kufungua njia ili masanduku ya kura yapakiwe kwenda kuhifadhiwa.
Full ulinzi.
Masanduku ya kura yakipakiwa garini.
Nikiripoti kutoka hapa Kirumbaaaaaa...ni mimi......
Mhe. Nderiananga akutana na Makamu wa Rais IFAD
-
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na
Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu
wa Rais...
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.