Shambulio hilo limetokea Jumamosi saa mbili usiku na hadi sasa inajulikana kuwa watu watano wamekufa, na wengi kujeruhiwa.
Mbunge wa jimbo hilo la Kamukunji, Yusuf Hassan, alisema alihisabu majeruhi 40 walipokuwa wakifikishwa hospitali ya taifa, ya Kenyatta. Wakuu bado hawakueleza nani alihusika na shambulio hilo; wala kama washambuliaji ni wa ndani au kutoka nje ya nchi.
Bwana Hassan alisema kuna majonzi na masikitiko mjini Nairobi kutokana na maafa hayo, lakini alisema safari za magari kwenye kituo zimeanza tena. Aliwasifu watu wa Nairobu kuwa shupavu.
Saa hizo za magharibi ni za harakati nyingi kwenye kituo hicho cha mabasi kutoka mikoani, na huwa na wasafiri wengi.
Chanzo bbc swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.