ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 25, 2012

MEDRICK SANGA KUSINDIKIZA UZINDUZI WA ALBUM YA VIDEO YA DANIEL SAFARI LEO KIRUMBA MWANZA

Mwimbaji wa muziki wa Injili toka mkoani Mbeya Med Medrick Sanga Leo anataraji kuzikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza pindi atakapo jumuika pamoja na wakazi hao kwenye uzinduzi wa album mbili za Video za Mwimbaji Daniel Safari waimbaji wote tayari wamekwisha wasili mkoa Mwanza kwaajili ya kuhudumu uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Uzinduzi wa Album ya Video ya Mwanadamu niMwanadamu yake Daniel Safari kutoka Dar es Salaam unafanyika leo katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ni kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni na hapa ilikuwa ni katika mahojiano kituo cha Television Barmedas Tv kutoka kushoto ni mratibu wa uzinduzi huo Albert G. Sengo, akiwa pamoja na mtangazaji wa kipindi Charles Sokoro katikati na mwimbaji Daniel Safari kulia.

Kwaya mbalimbali kutoka Mwanza zitahudumu leo ikiwa ni pamoja na Baptist Nyamanoro choir, Ufunuo P.A.G, P.A.G Patmo Choir, FPCT CITY Centre choir, Ebenezer FPCT Kitangili, Mwanza Gospel Choir, Jerusalem Choir Unguja, AIC Ilemela Choir, Umaki Kinamama Choir na nyingine nyingi.

Tamasha hili limeandaliwa na FPLUS ENTERTAINMENT Shukurani kwa wadhamini Rock city Tours LTD, GOLDCREST HOTEL, ZONGI PLUMBING ANDA GENERAL SUPPLIES, MBC HOT MEDIA, GLASS HOUSE, WATER HOUSE, VICTORIA DRIVERS ASSOCIATION, VICTORIA SECURITY SUPPORT NA SIX SOLUTION.
KARIBUNI SANA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.