ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 30, 2011

FIFA YAWASIMAMISHA BIN HAMMAM NA JACK WARNER.

Shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa, limewasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu, Mohamed Bin Hammam na Jack Warner baada ya kikao cha kamati yake ya maadili siku ya Jumapili.Suspended ... Qatar's Mohammed bin Hammam and Trinidad and Tobago's Jack Warner.

Shirikisho hilo sasa litaanzisha uchunguzi kamili juu ya madai kwamba wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean walipewa rushwa kupitia barua pepe iliyotolewa na kudai kuwa Mohamed Bin Hammam 'aliyanunua' mashindano ya mwaka 2022, ili nchi yake ya Qatar kupata nafasi ya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia. .

Maafisa wawili wa shirikisho hilo Debbie Minguell na Jason Sylvester pia wamesimamishwa. Lakini rais wa Fifa Sepp Blatter hakupatikana na hatia yoyote.


Sepp Blatter--->
Petrus Damaseb,makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili, alisema haya juu ya Bin Hammam na Warner: "tumeridhika kwamba kuna majibu tunayohitaji kuhusu suala hili."

Hata hivyo, Fifa imesisitiza kuwa hawana hatia kwa sasa hadi itakapothibitishwa kuwa walihusika katika sakata hilo. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufukuzwa kutoka shirikisho hilo na kupigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za mpira wa miguu.

Bin Hammam alikuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi ujao wa urais wa Fifa lakini alijiondoa mapema siku ya Jumapili.


Kwa hisani ya BBC swahili

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.