Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyotekea majira ya saa 7:30 usiku wa kuamkia jumapili ya mei 29, ambapo kundi la watu wakiwa na marungu, mapanga na sime walivamia mji huo na kutekeleza unyama huo.
Amewataja waliokutwa na mauti hayo kuwa ni Marwa Kige(66) na Mgosi Kige(58) ambapo inatajwa kuwa kabla ya mauaji kufanyika wauaji waliwateka na kuwatoa nje ya mji kisha kuwachinja kama mbuzi na walipohakikisha kuwa wamekufa walipora mifugo na kutokomea kusikojulikana. “Wakati Majangili hayo yakiteleza unyama huo kulikuwa na mtoto ambaye aliwaona nae hakusita kusimulia kwa jeshi la polisi mkasa mzima jinsi ulivyotokea,” alisema kamanda.
Aidha Kamanda amebainisha kuwa katika ufuatiliaji unaoendelea watu wawili wamekamatwa ambao ni Chacha Magori(19) na Mwita Magori(19) wote wakazi wa kijiji cha Kitunguruma wilayani Serengeti ambao wamekutwa na ng’ombe 7 kati ya 10 walioporwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.