Hali hiyo ilijitokeza jana kuanzia saa 7.30 mchana ambapo kundi hilo lilivamia kituo hicho na kuwazidi nguvu askari polisi waliokuwa ndani ya kituo hicho huku kundi hilo kutoka kijiji cha Itununu wakipiga kelele za kutaka watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuwachinja kama mbuzi watu wawili na kupora ng’ombe 10 ili nao wawamalize.
Kabla ya kuvamia kaunta ya polisi walikaa kikao nje ya uzio wa polisi ambapo kundi hilo ghafla likiinuka huku wakipiga mayowe na silaha zao tayari kwa vita.
Na wakati polisi waliokuwa kaunta wakiwa hawajui lolote kama mzaha wananchi hao waliingia ndani na kuzagaa mpaka nje kote wakitanda na kuanza kupaza sauti zao wakisema “Leo hatoki mtu mpaka tupewe watu wetu tuwamalize hapa hapa hawawezi
kufanya unyama hivi tukaachia,leo hatoki mtu,oooh,oooh,”
Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo akiwa amekamatwa na polisi wakimpeleka hospitali kwa matibabu.
Vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa zaidi ya saa moja zilipata sura mpya baada ya kamanda wa polisi wa wilaya hiyo Mng’ong’o aliyekuwa kwenye msafara wa naibu waziri wa Tamisemi Mwanri kufika akiwa na askari polisi wenye siraha na kuanza kufyatua hewani.
Kujitokeza kwa askari hao na kufyatua risasi kulipelekea kundi hilo kubwa kutawanyika na askari walikuwa ndani ya kituo na waliokuwa nje wakizuiliwa kuingia kupata nafasi ya kuchukua siraha na kuanza kupiga risasi za baridi na moto ovyo ovyo mpaka kwenye miji iliyoko jilani na polisi ambapo kuna watu zaidi ya watatu walijeruhiwa na kupelekwa Hospitali teule ya Nyerere.
Kwa karibu zaidi.
Kutokana na vurugu hizo askari polisi walilazimika kuziba barabara kuu ambayo hutumiwa na magari kwenda Bunda huku wakifyatua risasi za baraidi na kufanya mji mzima kuzizima kabisa.
Baadhi ya wananchi walikimbia na kutelekeza siraha zao za jadi na baiskeli ambapo vyote vimesombwa na kuhifadhiwa kituo cha polisi MUGUMU.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.