Nahodha wa AC Milan Gennaro Gattuso ameomba radhi kwa kumpiga kichwa kocha wa Tottenham Joe Jordan, baada ya timu yake kulazwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa timu 16 kuwania ubingwa wa Ulaya.Nahodha huyo wa AC Milaa mwenye umri wa miaka 33 ambaye siku za nyuma aliwahi kuichezea klabu ya Rangers ya Scotland, alizozana na Jordan mwenye umri wa miaka 59 na baadae akamsukuma kichwani. Sasa anasubiri kuadhibiwa kutokana na vitendo vyake vya utovu wa alivyoonesha uwanjani.
Awali alizozana na mshambuliaji wa Spurs, Peter Crouch na baadae akaoneshwa kadi ya manjano itakayomfanya asicheze mchezo wa marudiano, baada ya kumchezea rafu Steven Pienaar.
Mwisho wa mchezo, Gattuso alivua fulana yake na haraka akaelekea kumkabili Jordan, akimtolea maneno makali kabla ya kumpiga kichwa. Gattuso aliondolewa na wachezaji wenzake na akaacha ukali wake na kukumbatiana na mlinzi wa Spurs William Gallas.
Binadamu kuanza kuchimba madini angani?
-
Miamba ya angani ina utajiri mkubwa wa madini adimu kama platinamu, nikeli,
kobalti, na hata helium-3, ambayo ni muhimu katika uzalishaji wa nishati ya
nyu...
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.