Dr. SLAA
Maandamano yalianzia Kata ya Nyakato, Buzuruga na kupita barabara za Nyerere, Pamba, Kenyatta, Makongoro na hatimaye kuhitimishwa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa mkutano.
Mh. Sugu pale kati pembeni mwa diwani wa Mwaloni 'MBISHI'(sifa) Novat Manoko. Takribani wabunge 48 wanao wakilisha Chadema toka mikoa na wilaya mbalimbali hapa nchini wamehudhuria maandamano hayo na mkutano wake Mwanza.
Lengo la maandamano hayo ni kupinga serikali kulipa fidia kampuni ya Dowans, Kupanda kwa gharama za nishati na mfumuko wa bei ambao unapanda kila kukicha.
Nae mbunge wa Ilemela Higness Kiwia amewataka wananchi wa mkoa wa Mwanza kuondoa wasiwasi katika suala la ardhi kwani amekwishaongea na waziri wa ardhi na ameahidi kushughulikia tatizo hilo may mwaka huu.
Mbowe ambaye alionekana akizungumza kwa umakini mkubwa na kwa msisitizo, amesema yeye na timu yake wamekuja Mwanza kuwasha moto wa maandamano makubwa ya amani kwa muda wa siku tatu, leo katika wilaya za Nyamagana na Ilemela, kisha kuanzia kesho Ukerewe, Misungwi, Geita na Sengerema.
Aidha FREEMAN MBOWE amelipa shavu jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano ulioonyeshwa kwa kusimamia mkutano huo na hatimaye kumalizika kwa amani.
Mbunge wa jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje amehoji kama mikoa ya kanda ya ziwa ndiyo inayoongoza kwa raslimali na utajiri mkubwa kwanini wananchi wake wapigike kimaisha, amewataka wananchi kuanza mapambano ya kuhakikisha wanauaga umasikini kwa kushirikiana na viongozi wa chama hicho.
Sanaa nayo haikuachwa nyuma kuhusishwa katika kunakshi sherehe.
Chadema imempa Kikwete siku tisa kutoa tamko kuhusu ufisadi, Dowans na hali ngumu ya Maisha.
CHADEMA wamesema kuwa Moto kama huu wataendelea kuuwasha katika mikoa ya Mara, Shinyanga, Mkoa mpya wa Simiyu na hatimaye Mkoa wa Kagera.
Mwisho wa siku wananchi haoooo...warejea makwao kwa amani na utulivu hakuna aliyeumia wala kupigwa kwenzi licha ya umati kufurika katika maandaamano na uwanjani Furahisha.
Tupe maoni yako
Hongereni sana Viongozi, Wapenzi, Wanachama, na Wakaazi wa Jiji la Mwanza mmeonesha MSHIKAMANO WA HALI YA JUU na kumshushua KIKWETE, PINDA, NAHODHA, MWEMA, na ANDENGENYE kuwa mauaji yaliyotokea Arusha yalikuwa na mkono wa CCM, Polisi waliamua tu kuwaua raia kwa matakwa ya kisiasa, songeni mbele cha muhimu tusikurupuke twende kwa malengo tuwaamshe watanzania bila kuwaumiza watambue kuwa wanadhulumiwa na watawala wetu. MIKATABA MIBOVU, WIZI, UFISADI na utawala wa KISHKAJI usio na uwajibikaji USIO na MALENGO.
ReplyDeleteHaiingii akilini Mabomu yalipolipuka Mbagala mlitwambia ni makosa ya kiufundi hayatajirudia, lakini hata kabla hatujajengea makaburi ya ndugu zetu waliokufa yamelipuka mengine Gongolamboto na kuwaua ndugu zetu wengine, Waziri yuleyule, Wizara ileile, kwanini hajajiuzulu? ina maana hakumbuki alichofanya Baba yake kwa kile kisa kilichotokea Shinyanga? uroho tu wa madaraka, usijeshanga naye eti kajipanga kuwa RAHISI ajaye wa Tanzania!
HUSSEIN MWINYI UWAZIRI UMEKUSHINDA JIWAJIBISHE MWENYEWE KWA KAULI YAKO BAADA YA MABOMU KULIPUKA TENA.
Haiingii akilini kwenda kukodisha mitambo ya kufua umeme kwa bei mbaya wakati tunaweza kuinunua kwa bei ya chini, tunajua mmeweka cha juu na ndio maana hakuna mpango wowote wa kuliimarisha shirika la TANESCO, ili muendelee kulitafuna Taifa hili.
NGELEJA uwaziri umekushinda maana ulitwambia tatizo la umeme litakuwa HISTORIA NA KWELI LIMEKUWA HISTORIA
Haiingii akilini wawekezaji kufanya biashara Nchini mwetu bila kulipa kodi kwa kipindi cha miaka mitatu kisa kuvutia wawekezaji na ndio maana wengi baada miaka mitatu utasikia kampuni imeuzwa, wanachuma kisha wanaondoka mmetufanya majuha.
Mbona watanzania hawapewi miaka mitatu? Maana ukianzisha bashara tu hata kabla mwezi haujaisha TRA hawa hapa! WAMESHAFIKA! Waliotoka nje sawa wazawa hapana!
Sawa endeleeni lakini walahi mtalipa yooooote navyotuibia, MUNGU WA SASA NI KIJANA malipo ni HAPAHAPA.
Msichakachue maoni isipokuwa yale yenye matusi, vinginevyo maoni yayokuwa tofauti sisiem myaachie ili viongozi wetu watambue kuwa hatupendezwi na wanayofanya.
ReplyDelete