ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 24, 2011

MAANDAMANO YA CHADEMA YANAYOENDELEA SASA JIJINI MWANZA NI NOMA..

Chama cha maendeleo na demokrasia nchini CHADEMA leo kimefanya maandamano ya amani katika jiji la Mwanza kupinga kupinga mchakato wa uchaguzi na matokeo ya Meya wa Jiji la Arusha, kuunga mkono maandamano yaliyofanywa na chama hicho mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu na kupinga zoezi la serikali kulipa deni la Dowans.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Miamba muda huu wamejitokeza kwa wingi kuliunga mkono zoezi hili ambalo limeanzia eneo la Buzuruga wilaya ya nyamagana na kuelekea katika viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela ambapo kutakuwa na mkutano.

MabangozZZZ!!..

Hali ya hewa barabara ya Kenyeta.

Mmiliki wa dowans aka.....

Barabara ya Makongoro kuelekea kata ya Kirumba uwanja wa Furahisha eneo ambako mkutano utafanyika jioni ya leo.

Ujumbe kwa wakazi wa Gongo la mboto toka CHADEMA Mwanza.

Pikipiki eneo la kipita shoto cha ilipokuwa sanamu ya baba wa taifa.

Tupe maoni yako

18 comments:

  1. Mungu tunayemuamini na kumtegemea atatutetea Watanzania wote. Kila chenye mwanzo kina mwisho - hao Dowans watafika mwisho wao tu! Naamini siku moja Watanzania tutafunguka macho na kuchagua viongozi ambao watatetea haki za watanzania wote bila kuangalia rangi, dini, kabila. Hongereni sana Chadema - tuko pamoja. Poleni sana Gongo la Mboto - Mungu aliye mfariji mkuu na wafariji wafiwa wote pamoja na majeruhi wote.

    ReplyDelete
  2. HONGERA SANA CHADEMA KWA HILI UJUMBE UMEFIKA NA WATANZANIA TUPO PAMOJA NANYI...KWELI SASA TUMEAMINI VURUGU HUWA ZINALETWA NA POLISI NA SIYO MAANDAMANO..NAWAPONGEZA SANA UONGOZI WA POLISI MWANZA NA NA JESHI KWA UJUMLA...HII NDIYO DEMOKRASIA...ARUSHA NA KWINGINEKO WAIGE MFANO WA MWANZA...YA NINI KUMWAGA DAMU ZISIZO NA HATI??? BIG UP CHADEMA HONGERA KAMANDA MBOWE, DR SLAA NA VIONGOZI WENGINE WOTE WA CHAMA NA WATANZANIA WAPENDA DEMOKRASIA NA MAENDELEO..MUNGU IBARIKI TANZANIA UJUMBE UMEFIKA

    ReplyDelete
  3. this is good. big up kwa wana mwanza wote waliotoa support katika suala hili, good sign for our future, lazima kieleweke

    ReplyDelete
  4. Mwanza oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,Chadema juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, Police mwanza oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, nawapa big up sana wapendwa wote wa Mwanza kwani mmefanya la maana, zaidi viongozi wetu na Rais wetu slaa na mwenyekiti wetu Mbowe nawapa big up sana,endeleeeeeeeeeeni hivyo hivyo serikali itambuwe tulivyowachoka kwa ufisadi wao

    ReplyDelete
  5. nguvu ya umma hiyo..............

    ReplyDelete
  6. Hongera lakini mimi na shauri si kila siku kuwa na maandamo maana hata kama mnania njema kuandamana kila siku siyo nzuri

    ReplyDelete
  7. Mwanza oyeeeeee mwanza juuuuuu! Napenda kutoa Comment zangu kama nilivyo waona wenzi wangu nawao wametoa za kwao. Hii ni kwa mtanzania yeyote ambaye ama hajakata tamaa ya maisha au anaiangalia tanzania ya siku za usoni. sio kila kingaacho eti ni dhahabu hapana, na kwa kupitia nguvu ya uma tunaweza kuitoa serikali iliyopo madarakani. swali langu ni hili, tukishaitoa serikali iliyopo madarakani tukaweka chama hiki kilinacho tufanya tuandamane baada ya muda mchache tukaona kuwa hawa nawo wanatufanyia ndivyo sivyo tutakapo taka watoke ili tuweke wengine hawatatoka, je watanzania tmeshakua tayari kufa! kwakua hawa watatuua kama kuku hawa hawana lolote zaidi ya kuwa nao wanataka madaraka. nawao pia hawataweza kutimiza matakwa ya watanzania uongo mtupu watanzania wenzangu tukae chonjo na watu wa aina kama hii. Serikali iliyopo madarakani napaswa kuzichukua hizi ikiwa ni challenge na kuzifanyia kazi kisha kujikosoa na kujirekebisha imetufanyia mazuri lakini pia na mabaya yapo hizi ndizo fursa za serikali izitumie kujirekebisha nashukuru sana nimependa utulivu na uvumilivu mkubwa walio uonyesha polisi jana vinginevyo kwakasoro ndogondogo zilizotokezea kama polisi wasingezivumilia sasahivi tungekua tunaongea mengine

    ReplyDelete
  8. Maandamano yanapendeza yakifanyika kwa amani kama ambavyo mkoa wa mwanza umeonysesha mfano,hongera jeshi la polisi mkoa wa mwanza.

    ReplyDelete
  9. CHADEMA WOTE NI WASENGE, MNAANDAMANA BILA MPANGO,NA MWAKA HUU LAZIMA HIKI CHAMA KIFE KAMA ILIVYOKUFA NCCR-MAGEUZI- MMBWA NA MAPAKA NYIE

    ReplyDelete
  10. Nadhani huyu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza anafaa zaidi kuwa IGP ameonesha umahiri katika kazi yake, Mwema unapashwa kujifunza toka kwa KAMANDA SIRRO, wala usmuonee gere, hakuna maafa wala mabomu, wala fujo. Hongera CHADEMA, hongera wana Mwanza kwa maandamano ya AMANI.

    ReplyDelete
  11. Ona government inavo jichangana, inamana sahivi hakukuwepo habari za kiinterestia? ya Arusha ya gvt, heko chadema we believe in it!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. Viva CHADEMA SAIDIENI KUPOFUA MACHO YA WATANZANIA! WE ALL NEED A NEW AND BETTER TANZANIA THAT CARES FOR HER PEOPLE!

    ReplyDelete
  13. Nadhani nimeelewa vema comment yako kuhusiana na maandamano ya Mwanza kuwa tunaweza kuitoa serikali iliyopo madarakani kupitia maandamano,nadhani mtoa hoja hapo juu hujaelewa maana au dhana nzima ya maandamano,mimi sio mweledi sana katika siasa lakini naelewa kuwa maandamano lengo kubwa ni kufikisha ujumbe kwa walengwa na siyo lazima kuigóa serikali iliyopo madarakani,maandamano yamekuwa yakifanyika mara nyingi na ya aina tofauti kumbuka DUNIA YA LEO NI KIJIJI huwezi kumdanganya mtu kama tunavyodanganywa sasa hivi na viongozi wetu wengi wanaohubiri kunywa maji wakati wao wanakunywa mvinyo kwa kasi

    ReplyDelete
  14. kama misri na libya...

    ReplyDelete
  15. TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA IMESHINDIKANA GADAF LIBYA AMBAKO AFYA,NA ELIMU BURESEMBESE KIKWETE TANZANIA AMBAKO WENYE VX NI WATOTOT WA WAHESHIMIWA NA WAKE ZAO.

    ReplyDelete
  16. USHAULI WANGU KWA MUHESHIMIWA KIKWETE ANGALIA WANANCHI WAKO WANACHOHITAJI NINI UWAFANYIE C.C.M ISIJE KUPOROMOKA MIKONONI MWAKO ANGALIA BARABARA ZISIVYOJENGWA KWA UBORA..TAZAMA KIPANDE CHA KUTOKA AIR PORT KWENDA GONGOLAMBOTO KINAVYOCHUKUA MUDA MREFU KINACHOFANYIKA HAKUNA...ANGALIA UMEME KWA NINI HICHI KIANGAZI WATU WASITOE MATOPE KATIKA MABWAWA NA UJENGE JINGINE KUBWA ILI UVUNE MAJI KIPINDI CHA MASIKA AU HAIWEZEKANI????ANGALIA WATU WANVYOVUNJIWA NYUMBA ZAO KWA MRADI WA MTU MMOJA JE HAYO MABASI YAENDAYO MWENDO KASI MTAYAWEZA??BARABARA ZENYEWE ZIKO WAPI AU SERIKALI INAKURUPUKA TU????HIVI HUONI WANANCHI WAKO WANAVYOISHI KWENYE NYUMBA ZA MIAKA 47????HUONI KIJIJINI WANANCHI WANAVYOTEMBEA BILA NGUO NA VIATU????HV HOUNI WANAFUNZI WANAVYOKOSA HATA MADAWATI YA KUKALIA???????HIZO PESA MNAZOCHANGISHA WAKATI WA KAMPENI KWA NINI MSIZIFANYIE KAZI WAKATI HUU??NA HILI DENI LA DOWANS LINA UMUHIMU GANI KULIPWA??NA MADINI YETU YANAENDA WATU KODI ZETU ZINAENDA WAPI???HV UTAWAFUMBIA MACHO HAWA MAFISADI MPAKA LINI WANAKUCHAFUA HAO ANGALIA 2005 ULIVYOPITA KWA KISHINDO LAKINI ANGALIA SASA WANANCHI WANAZIDI KUPOTEZA IMANI...AMKA IKIWEZEKANA FUATILIA MWENYEWE UPUNGUZE SAFARI ZA NJE ILI WANANCHI WARUDISHE IMANI NA SERIKALI YAKO

    ReplyDelete
  17. CHADEMA HOYEE 2015 IKULU

    ReplyDelete
  18. maandamano ni changamoto kwa serikali ila ni kweli yatasaidia kusinikiza umeme uweze kurudi. kwa mimi binafsi nina mingi kichwani mwangu ambayo nahisi kama watanzania wataandamana kwa hayo itakua ni hoja ya msingi zaidi.
    jambo la maana kwanza ni kutazama mfumuko wa bei za kilakitu tukianzia kwenye huo umeme nauli za mabasi ya mikoani kuwa juu tofauti ya thamani ya pesa ya kitanzania ukilinganisha na za kigeni. uchumi wote kwa ujumla katika kila secta umeguswa.
    hao wapinzani watezame mstakabali wa tanzania kwa busara zaidi na sio kisiasa kama wanavyofanya.
    moblisation kama hiyo ifanywe kwa mstakbali muhimu ambao utakaobadilisha taifa zima.
    kupinga matokeo ya uchaguzi kweli lina tija mpaka watu kuuwana?
    sengo tutazameni mambo kwa umakini zadi

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.