Mbwa huyu sijajua kitu gani kilimsibu hata akawa katika hali hii ya mguu wake mmoja wa mbele kusagika kabisa kiasi cha kuning'inia hivyo kumwacha katika hali ya kusikilizia maumivu saa zote. Kama utamkuta katulia basi kapata muda nayo maumivu yamepungua kauchapa usingizi, akiwa macho ni kugugumia kwa maumivu mwanzo mwisho. Wadau wanao ishi eneo hili karibu na Tilapia hotel Mwanza (mahala ambapo anazurura) wanasema kuna kipindi mbwa huyu huwa anabweka kwa hasira huku akirukaruka akiungata kwa ghadhabu mguu wake yaani kwa ufupi ANAUTAFUNA kama nyama. Ukiutizama kwa karibu mguu wake huu umeoza... sijui ni kansa imempata!? yaani sijui... Nimejaribu kuuliza wadau kila mmoja anasema kivyake..... Hebu tujiulize nini matokeo, ni balaa gani linaloweza kufuata mara baada ya hapa? Hakika tutaumia.
Idara ya wanyama/mifugo sanjari na wadau husika naomba kuwakilisha.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
Mkuu kumbe huyu bwana dog ulimuona...yuko mza mjini anazunguka zunguka tu kitakuwa ni mambo yao ya starehe...wakamtafuna wenzie..
ReplyDelete