ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 2, 2011

TIGO KANDA YA ZIWA YAUKARIBISHA MWAKA KWA KUMWAGA ZAWADI KWA WAFANYAKAZI WAKE.

Katika kutia changamoto kwa wafanyakazi wake kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa simu za mkononi Tigo imefanya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2011 tarehe 1january2011 katika viwanja vya BOT pansiasi jijini Mwanza.

Washiriki wa hafla hiyo iliyofana walikuwa ni wafanyakazi wa kampuni hiyo toka mikoa yote ya kanda ya ziwa ambapo humo ndani zawadi kwa wachapakazi bora na wanamichezo bora zilitolewa.

Kombaini ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Mara upande wa netibali ilipata ushindi na kukabidhiwa kombe baada kuinyanyasa timu ya kombaini ya mikoa ya Tabora, Kigoma na Bukoba.

Kombaini ya Mwanza, Shinyanga na Mara (red) ikipata bao.

Mchezo wa soka ulichezwa baina ya Timu ya Tigo Kombaini ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Mara (red) iliyobanjuliwa kwa kisago cha aibu 4-2 toka kwa kombaini ya Tigo mikoa ya Tabora, Kigoma na Bukoba(blue).

Washindi wa Tigo soka mikoa ya Tabora, Kigoma na Bukoba na kombe lao.

Bendi ya muziki wa dansi inayotikisa kanda ya ziwa Okestra Kamanyola walikamatisha na kupagawisha wafanyakazi nowma.

Kila mmoja alitoka na Tabasamu kwa mazawadi yaliyomwagwa ndani ya hafla. Meneja Matangazo na Promosheni, Redemtus Masanja (kushoto) akikabidhi zawadi.

Wafanyakazi wa Tigo mikoa ya Kigoma, Bukoba na Tabora kiukweli katika suala la style za ushangiliaji walifunika, hapa ni shangwe kwa moja ya wadau wao aliyejinyakulia Mountain bike.

VutaaaaaaaaaH!! Mwisho wa siku kombaini ya mchezo wa kamba mikoa ya Tabora, Kagera na Kigoma ikawazidi nguvu na kuwabwaga Mwanza Shinyanga na Mara pichani walioanguka.

Utaratibu wa zawadi ulikuwa ni ngazi kwa ngazi nao ulitwaliwa kama changamoto kwa wenye bidii kuongeza juhudi na maarifa kazini na kwa wengine kutobweteka. Pikipiki hiyoo wazeya ikiondoka.

'Sipati picha jinsi geto patakavyotisha' Ni mwanadafada kutoka Bukoba akivuna alichopanda kwa kunyakua saundi, na hapa akikabidhiwa toka kwa meneja mawasiliano kanda ya ziwa Joseph Mtalemwa.

Wau mzobemzobe!! style ya kulikwea jukwaa kunyakua zawadi.

Television hiyooooo kwa dada wa tigo Shy-town.

Usafiri kwa shughuli binasfi na ufanisi wa kazi hata sehemu zenye vilima mbele ya 'mountain bike' aaaaaH! halivuji jasho.


Michezo ni burudani michezo ni afya, Washindi wa michezo ya jumla TBR,KG na BK na shangwe zao.

Makamuzi ya ONE N' TWO na Dj Chriss toka Villa park.

KATIKA mahojiano yake na vyombo vya habari Meneja Matangazo na Promosheni, Redemtus Masanja alisema "Tukio kama hili tunalifanya kila baada ya miezi sita nia na madhumuni ikiwa ni kuhamasisha na kuchochea utoaji wa huduma bora tena zilizo makini kwa wateja wetu haiishii hapo bali hata kuona yale malengo yetu yanafikiwa kwa kasi aina gani. Sasa kwa wale wanaofanikisha na hatimaye tukaona juhudi zao hatuna budi kuwaonyesha kwamba wanachokifanya tumekiona hivyo tunawatunuku zawadi na kuwawezesha ili kusukuma mbele gurudumu letu la maendeleo. Na kwa wale watakaokosa zawadi, nafasi ipo waongeze juhudi kamwe hatuto wabania."
Wadau wa habari kutoka Star TV Mwanza James George (kushoto) na Ben Star wakifukunyua zana za maangamizi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.