ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 16, 2012

4th EDITION INTERNATIONAL TUBINGEN AFRICAN FESTIVAL 2013, CALL FOR ARTSTS AND EXHIBITORS

Enie-Muyang-Tatah-founder and CEO

header top

4th Edition International Tubingen African Festival 2013, near Stuttgart –South Germany

more than just a festival! Open Call For Artists and Exhibitors

4 newsletter

Business, Sport, Music, Market, children and youth village…
The International African Festival Tubingen, known as AFRICACTIV, has grown from a local to international audience, striving for quality. The vision goes beyond just a festival of cultural celebration to promoting African investments on a bilateral strategy by creating a market for SME African enterprises to penetrate the European market with products such as handcrafts, textile and designs, fashion and beauty as well as exposing the competence of African scholars in all works of arts - literature, theater, music, film etc.
AFRICACTIV, a culture of family
4 newsletter2
  
This event is especially dedicated to the African Diaspora world-wide “It harnesses a unique culture of family, an embodiment of togetherness, passion of good music and charms. Our program offers the opportunity for Africans world-wide to take a holiday in Tubingen. Our programs are tailored made to suit every need and public -families, kids and youths, students, entrepreneurs… The festival is compacted and displayed on the beautiful meadow at the Tubingen festival ground, giving you the opportunity to enjoy the festival thereby throwing an eye on your kids.
4 newsletter3
Tubingen is a beautiful University city located in the south of Germany, near Stuttgart
Tubingen is known as the home of scholars. It has a remarkable culture - a replica of Zanzibar. Since 2010, a group of Africans resident in this area, decided to make Tubingen a holiday place for all African diaspora to meet and celebrate our culture. Last years celebration – the 3rd Edition hosted more than 15.000 visitors world-wide a grandiose occasion that took place for 4day presentating a true picture of africa. The 4th Edition is currently being planned for thursday 8th to Sunday 11 of August 2013 - 4days nonstop, 30.000 diaspora world-wide will attend this event, so be there!
International Diaspora Award – Final call for artist 2013
4
newsletter4
Register now, sending a live video about your band per mail
This program is a showcase of Africa´s young talents and dynamism, each year we give out awards to Africans in every works and fields – Music, photography, designers, literature and more as a compensation for hard work and creativity. African traders, musicians, writers, photographers, designers, companies and entrepreneur, African football associations etc…from anywhere in the world are welcome to apply for opportunities to showcase their talents: Register, participate and win an award, all free of charge!

Music (Bands and groups with at least 5 musicians)

Music genre (African – Soukouss,Bongo Dance "Muziki wa Dansi" Makossa, high-life, Meringue etc, Reggae, Zouk, Samba,)

Drumming; Traditional dance groups, theater, acrobatics – associations and schools
Help keep AFRICACTIV –Festival (Entry free!)
This festival shall be FREE ENTRY to all the Diaspora and the public despite the high cost, thus providing access and the possibility for all Africans to get together without inflicting extra cost on them, especially those travelling from far. You can help keep this festival entry free by your freewill donation, sponsorship (public / private) be a volunteer.

Your benefits as a sponsor / donor/ Volunteer is a win-win situation by inserting your logo on the festival flyers, banners, posters, homepage and newsletter, 15.000 visitors attended the 3rd edition 2012, and at least 50.000 are expected to attend 2013 at the 4. Edition The festival has a magazine called (AFRICACTIV- MAGAZIN).
This magazine reports about the festivals program and the activities of the Diaspora in the south of Germany. It´s a non-profit project and generates its funds by providing places for advertisement. It has 20.000 copies that are distributed free of charge in all local African shops, businesses, and tourism and travelling agencies as well as households. We appreciate your contribution and support by placing your advertisement in our magazine.
Contact us- AFRICACTIV e.V
Tel: +4915210610374

Monday, October 15, 2012

ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA MAREHEMU BARLOW AAGWA NA MAELFU UWANJA WA MICHEZO NYAMAGANA LEO

Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow ukiandaliwa kushushwa toka katika gari maalum lililoubeba mwili huo kutoka Hospitali ya rufaa Bugando kwenda nyumbani kwake kisha uwanja wa Nyamagana ambapo ibada ya kuuaga mwili huo imefanyika.


Askari wa vikosi maalum wakiulaki mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mwanza Liberatus Barlow.


Kwa mwendo wataratibu kikosi maalum kikiwa kimeubeba mwili wa marehemu Barlow kuupeleka mahala maalum pa ibada na heshima za mwisho kwa wakazi wa kanda ya ziwa.


Matayarisho ya ibada yakifanyika.

Hii ni Familia ya aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Marehemu Liberatus Barlow kutoka kushoto ni...(Majina yaja)


Safu ya Jeshi la wananchi na wawakilishi wake msibani hapa.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo  alisema kuwa Kamanda Barlow alikuwa ni kiongozi wa mfano na alikuwa mhimili mkubwa katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kutokana na kutoa michango mbalimbali muhimu ya namna ya kudhibiti masuala ya uhalifu muda wote.


Makamanda wa jeshi la polisi wakiwa wamesimama kusubiri hatua 


Eneo la jukwaa kuu viongozi mbalimbali ndani ya  uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. 


Maelfu ya wananchi waliofurika kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kamanda wao.

Akiongoza misa hiyo Paroko Raymond amesema kuwa tukio la kuuawa kwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow linapashwa kulaaniwa na kuwataka waumini wa dini mbalimbali kuwaombea wale waliofanya tukio hilo ili watubu kwani wamefanya kitendo ambacho sio cha kiungwana.
Misa imefanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana ikiongozwa na paroko wa kanisa la Nyakahoja Father Raymond Manyanga wa shirika la SJ na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wandamizi wa serikali wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa, Wakuu wa wilaya, Viongozi wa dini pamoja na wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa.


Waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu,Bunge, sera na uratibu William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow, katika ibada maalum iliyofanyika uwanja wa Nyamagana.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akitoa heshima kwa kamanda wa polisi mkoa wake marehemu Liberatus Barlow aliyeuawa majuzi na watu wasiojulikana.
Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Robert Kanumba (mbele) akiongoza msafara unaopita kutoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow. 


Lawrance Masha ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa  (NEC - CCM)  wilaya ya Nyamagana akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow.


Masista kutoka Parokia ya Nyakahoja wakitoa heshimazao za mwisho.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Joseph Kasheku Musukuma akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Magu Jaquline Liana wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa polisi Mwanza Liberatus Barlow.


Mbunge wa viti maaalum (CCM) Maria Hewa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza. 

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC - CCM) wilaya ya Tarime Christopher Gachuma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow.


Mbunge wa Rolya Lameck Airo akiongoza wabunge wenzake kuuaga mwili wa marehemu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mwanza Liberatus Barow.


Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji mafuta ya MOIL Altaf Hiran Mansoor 'Dogo' akitoa heshima zake za mwisho.
Nyamagana ground.

Mfanyanyabiashara ambaye pia ni kada wa CCM kata ya Kirumba Jackson Robert 'Jack Fish' akitoa heshima zake kwa mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow.


Maafisa wa jeshi la wananchi walipata fursa pia kutoa heshima zao.


Maafisa wa jeshi la wananchi walipata fursa pia kutoa heshima zao.


Mwili wa marehemu Barlow unatarajiwa kusafirishwa leo jioni kuelekea nyumbani kwake Ukonga jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa na ndugu na jamaa zake kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake Koro wilaya ya Moshi vijijini kwa ajili ya mazishi.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

KAMANDA BARLOW KUAGWA LEO JIJINI MWANZA.

Enzi za uhai wake Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow (kulia) hapa alikuwa akitoa ahadi kuchangia mfuko wa Umoja wa wanawake wajasiliamali ulioanzishwa jijini Mwanza ujulikanao kwa jina la KWEA ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alikuwa ndiye mshereheshaji. 

Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la Polisi Mwanza, Marehemu Liberatus Barlow utaondoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando saa 1:00 asubuhi ya leo na kupelekwa nyumbani alikokuwa akiishi marehemu eneo la Pasiansi jirani na kotaz za Marine Service.

Baada ya kufikishwa kwenye makazi hayo mwili huo utakaa kwa muda wa dakika 30 kisha utapelekwa viwanja vya Michezo Nyamagana ambapo kuanzia saa 2:30 Fursa itatolewa kwa viongozi wa kada mbalimbali na wananchi kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza na mikoa jirani kutoa heshima zao za mwisho kwa mchapakazi huyu aliyeiaga dunia katika mazingira ya kutatanisha.
  
Baada ya zoezi hilo kukamilika kwa nafasi yake mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow utaondolewa kwa msafara hadi Airport Mwanza ambapo utasafirishwa kwenda nyumba ya marehemu jijini Dar es salaam ambako familia yake inaishi.

Kesho (jumanne)  zitafanyika lojistics mbalimbali ikiwa ni pamoja na  Maofisa wengine wa jeshi la polisi Makao makuu (jijini Dar es salaam),  wananchi, majirani na marafiki kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kamanda Barlow, kisha mwili utasafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro hatimaye Marangu kijijini kwao kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumatano.

Kwa hivi sasa viongozi mbalimbali wamekwisha wasili jijini hapa kwaajili ya taratibu za leo tangu juzi tunaye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi, tunaye pia mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI Robert Manumba na timu yake, viongozi wengine ambao walikuwa kwenye mbio za mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga Mh. Asha Rose Migiro na wengine wengi. 

TANZANIA YAPATA SHUJAA MPYA

Wilfred Moshi akipeperusha bendera ya Tanzania kileleni Mlima Everest

Wilfred Moshi safarini kuelekea kileleni

Mike Knox mwanzilishi wa Twende Pamoja akifanya mazungumzo na Urban Pulse

Mwanzilishi wa Twende Pamoja Mike Knox akila pozi na Frank Eyembe wa Urban Pulse Edinburgh, Scotland 

Mh Peter Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya TWENDE PAMOJA. Kutoka kushoto Lee Patterson, Mike Knox (Director) Wilfred Moshi, Mary Iannarelli, Fiona Macpherson na Veronica Avinou

Safari ya kukwea Mlima Everest ikipamba moto

Wilfred Moshi akifanya mahojiano na Urban Pulse katika kilele milima ya Volcano Holyrood Park Edinburgh

Frank Eyembe wa Urban Pulse na Wilfred Moshi baada ya kupanda moja ya milima mirefu Uingereza iliyopo Holyrood Park Edinburgh

Imeandikwa na Freddy Macha kwa ushirikiano na Urban Pulse
Picha zote hisani ya Wilfred Moshi na Urban Pulse
 Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi yetu kijana Wilfred Moshi, Mbongo wa kawaida tu (anayefanya kazi ya upagazi kuwahudumia watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro), ameweka rekodi mpya ya kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda Everest - mlima mrefu kushinda yote duniani.

 Hivi karibuni, Moshi,   alialikwa majuma matano nchini Uingereza kutembelea shule mbalimbali za Scotland akakutana na takribani wanafunzi 5,000 .

Wanafunzi walitaka kufahamu namna alivyopanda mlima Everest wenye mita 8,848 (futi 29, 029). Mlima huu mgumu kuukwea kuliko yote ulimwenguni umewahi kupandwa na na watu 4,000 toka ulipoanza kufikiwa kileleni na Edmund Hillary na Sherpa Tenzig Norgay mwaka 1953. Kati ya hao 200 walifariki. Mwaka huu wanne wameshafariki wakiijaribu shughuli hii inayochukua  miezi miwili na kugharimu Dola 100,000 (Shilingi milion 157,500,000) Linganisha na mlima Kilimanjaro unaodai  siku tano na gharama (ikiwepo vifaa husika) Dola 2,000 (Shilingi milioni 3, 161).

Wilfred Moshi ni Mtanzania wa kwanza na Mwafrika wa tatu kufikia kilele cha kitendawili hiki Mei 19 2012 (kilichoitwa “Chomolungma” na wenyeji kabla ya kubatizwa jina la Everest na Waingereza enzi za ukoloni)  
Wilfred aliyezaliwa mwaka 1979 na kumaliza kidato cha sita shule ya Kilimanjaro Boys, amekuwa akipanda mlima Kilimanjaro tangu angali bado shuleni na miaka 19.

Mara baada ya kuwasili Edinburgh, Scotland alikaribishwa bungeni akakutana na Waziri wa Sheria mheshimiwa Kenneth MacAskill na viongozi wengine. Safari ilikirimiwa na shirika la “Twende Pamoja” lililoanzishwa na Mike Knox miaka 30 iliyopita. “Twende Pamoja” imejenga ushirikiano kati ya wanafunzi wa Scotland na shule 34  za Kitanzania. Ni moja  ya mashirika, watu binafsi  na wafadhili mbalimbali ulimwenguni waliochangia fedha za kumwezesha Moshi kupanda mlima Everest.

Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe vile vile alisafiri toka London kumtembelea Wilfred Moshi na kumpa heko. Umbali wa London had Scotland ni kama Dar es Salaam hadi Kigoma!
Kwanini Moshi anahusudu kupanda milima?

Ukweli sisi bado hatuoni umaana (au umuhimu) wa kupanda milima. Anasema lengo lake lilikuwa kutimiza ndoto ya Mtanzania wa kwanza kupanda Everest. Pili, upandaji milima ni moja ya njia zinazoweza kusaidia kujenga jamii kwa misaada na fadhila za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO). Tujiulize vipi alisaidiwa na watu wengi namna hiyo kuchangia fedha takikana? Tatu, Moshi amethibitisha ukiwa na moyo na jitihada unaweza kufanya lolote. Ushujaa na ushupavu wake utasaidia kuwahamasisha Watanzania kuwa ukitaka kufanya jambo lolote lile unaweza ili mradi uwe na moyo na nidhamu.

Mpanda milima mashuhuri, Mike Hamill, aliyeshakwea milima yote  mikubwa saba duniani anasema katika kitabu chake kipya (“Climbing Seven Summits”) wapanda milima ni watu wenye moyo wa kufikia malengo na kufanikiwa katika maisha yao.

 Akiwa Uingereza Moshi alipanda mlima wa Ben Nevis  mrefu kuzidi  nchi hii-  wenye mita 1,344 (futi  4, 409). Baada ya kuimudu milima mitatu sasa , Wilfred Moshi ameazimia kupanda milima  katika mabara yote 7 duniani. Anasema amebakisha milima mitano: Aconcagua ( Marekani ya Kusini ), Kosciuszko (Australia), Vinson Massif ( Antarctica) McKinley(Alaska) na  Elbrus(Urusi).

Mungu ambariki Mtanzania huyu mwenye jazba na hamasa anayetuletea sifa.
Soma habari zaidi:

TPBC YAMUENZI BABA WA TAIFA “MWALIMU NYERERE”



 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
OCTOBA 14, 2012
 
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inachukua fursa hii kumuenzi baba wa taifa “Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” wakati Tanzania inaadhimisha miaka 13 ya kifo chake. Juhudi za mwalimu katika kuleta maendeleo ya michezo pamoja na haki, usawa na ushirikiano kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutazienzi daima.

TPBC inakumbuka na kuenzi mchango wa baba wa taifa katika tasnia ya michezo hususan ngumi za kulipwa nchini tukikumbuka kuwa ni miaka ya mwisho ya utawala wake ndipo ngumi za kulipwa zilianza rasmi Tanzania mwaka 1982.

Juhudi za baba wa taifa za kuendeleza michezo zilikuwa na sura mbili kubwa:

Sura ya kitaifa: Michezo wakati wa utawala wa baba wa taifa ilianzia kwenye shule za msingi na kwenye vitongoji na hivyo kuwapa nafasi nzuri watanzania wengi wakati mzuri sana wa kushiriki na kuchangia kwenye maendeleo ya michezo.

Hii ilisaidia watanzania kujenga ari na vipani vya michezo ambavyo huanzia kwenye umri mdogo na hivyo kushiriki kwao kwenye michezo kuanzia shule za msingi na vitongoji kuliwapa nafasi nzuri ya kujijenga kimichezo.

Umri mzuri unaotakiwa kuanza kujishughulisha kwenye michezo ni kuanzia miaka 7 na kuendelea. Mtu anapoanza kujishughulisha kwenye michezo mapema akiwa na umri mdogo huweza kuonyesha na kuendeleza kipaji chake mapema na kwa hali ya juu.

Baba wa taifa alijenga msingi wa umoja na usawa ambao uliwezesha watanzania wote kushiriki katika michezo bila ubaguzi wa ukabila, udini na jinsia jambo ambalo halikuwa rahisi kwa nchi nyingine wakati ule.

Sisi tumejionea miaka ya karibuni kwenye michezo ya Olimpiki iliyomalizika katika jiji la London, Uingereza baadhi ya wanamichezo wa jinsia moja ndipo waporuhusiwa.

Hivyo baba wa taifa aliwezesha watanzania wote kushiriki kwenye michezo bila ubaguzi.

Sura ya Kimataifa: Serikali ya baba wa taifa ilijenga msingi imara kwa vyama vya kitaifa vya Tanzania kujiunga kwenye na mashirikisho mengi ya kimataifa kama vile CECAFA, Olimpiki, FIFA, AIAA, IBF, WBC, WTA na mengine mengi.

Uanachama huu watanzania kwenye mashirikisho haya uliweza kujenga misingi ya “Utalii wa Michezo” kwa Tanzania kujulikana duniani na hivyo kuwezesha nchi kutangaza vivutio vyake vya utalii na mahala pazuri pa kuwekeza.

Ni wakati wa utawala wa baba wa taifa mchezo wa riadha uliweza kuitangaza sana Tanzania katika medani ya kimataifa.

Jambo hili halina budi kuigwa na kuendelezwa na awamu zilizomfuata mwalimu hususan awamu ya sasa.

Sisi tunafikiri kuwa wakati rais wa sasa wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kiongozi wa kwanza mbali na mwalimu kuwekeza juhudi zake binafsi katika kuendeleza michezo, wale waliopewa jukumu la kusimamia tasnia hii hawana budi kumsaidia kuzifanya juhudi hizi zizae matunda.

Tunachukua fursa hii adimu ya kumuenzi baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika juhudi zake za kuendeleza michezo katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Uongozi wa TPBC ni:

Rais: Onesmo Alfred McBride Ngowi
Makamu wa Rais: Godfrey Madaraka Nyerere
Katibu Mkuu: Nemes Kavieshe
Katibu Mkuu Msaidizi: Nicholus Mallya
Mwenyekiti wa Viwango na Ubingwa: Boniface Wambura
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji: Mark Hatia, Henry Mfinanga, Michael Buchato,


Imetolewa na Uongizi:

Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais,  
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)

Sunday, October 14, 2012

MASWALI MENGI YAIBUKA KIFO CHA KAMANDA WA POLISI MWANZA

Marehemu Kamanda wa polisi Liberatus Barlow.
1. Endelea kufananisha picha. Lakini endelea pia kujenga mashaka kama nilivyoandika siku mbili zilizopita.

2. Kamanda alikuwa anatoka wapi - sherehe?

3. Alimbeba nani - mwalimu? Lifti? Kutoka wapi kwenda wapi? Mwalimu alikuwa anatoka wapi usiku huo? Hajaolewa? Mume wake yuko safari au alighairi sherehe? Mume wa mwalimu ni nani? Wanaishi wapi? Alimwacha wapi mume wake na kubebwa na polisi mkuu wa mkoa? Aliwaacha wapi aliokuwa nao na yeye kupata lifti? Kwanza kabisa, alikuwa na nani kabla hajapewa lifti. Mtu wa mwisho kumwona mwalimu na polisi wakiondoka ni nani? Kama polisi alipakia abiria wengine walishuka wapi?

4. Mkuu wa polisi na mwalimu walikuwa pamoja kwa muda gani wakiwa peke yao na wapi? A La Kairo au wapi? Hapo Kairo walikuwa wakifanya nini - tangu lini hadi lini? Mwalimu wa shule ya msingi ya Nyamagana, eti? Alikuwa anatoka wapi - naye kwenye sherehe hiyohiyo na Burlow?

5. Mwalimu mkuu anasema nini? Dada yake? Ndugu zake wengine? Hivi polisi mkuu wa mkoa na mwalimu walikutana kwa bahati mbaya? Tafuta. Tafuta. 

6. Mahali aliposhambuliwa mkuu wa polisi ni karibu na kwake au kwa mwalimu?
7. Endelea kujenga mashaka: Ofisa uhamiaji aliyenusurika yuko wapi katika sinema hii? Hajui lolote? Kati ya polisi mkuu na mwanamke, hakika hakuna pandikizi la kukamilisha sura ya sinema? Hakuna?????? Tafuta. kama lipo linaweza kuwa limewekwa na nani na kwa nini?

8. Katika miaka mitatu iliyopita: Angalia kesi mahakamani Mwanza. Hakuna nyingi zinazohusu polisi na nyendo zao katika maisha ya familia mbalimbali? Hii ishu ya Burlow yaweza kuwa moja ya hizo? Uliza mahakimu - wamelalia malalamiko kwa kuwa polisi wamelalia uchunguzi na ushahidi? Tafuta.

9. Yuko wapi mke wa polisi mkuu? Hakwenda kwenye sherehe? Alikatazwa? Hakupenda? Alijisikia vibaya? Hayupo Mwanza? Yuko wapi.

10. SINEMA HII INAFANANA NA ILE YA UDAKU. SIYO! Acha vijana wafumue muone kitakachotoka kichakani. Na hicho ndicho mazoea, tabia na sasa utamaduni. 

11. Kumbuka Burlow alitoka mkoani Mara na mkondo wa wakimbizi na wahamiaji na utajiri wao, kama nilivyoeleza katika disipachi iliyopita, vina nafasi katika mahusiano na tabia za polisi na uhamiaji. Nani atajinyofoa katika hili lenya urefu na upana wa dunia.

12. Naomba Katu na wengine, mwendelee kuchimba. Kama kweli Burlow amefariki katika mazingira hayo, nasema kuna jambo ambalo halina nyumba maalum. Liko kila nyumba ya mwenye madaraka; mwenye fedha za nyongeza. Bali alale pale ambako Mwenyezi Mungu atapenda.

NDIMI:-
Ndimara Tegambwage
Information and Media Consultant
P.O. Box 71775, Dar es Salaam
Tel: 255 (0)713614872
e-mail: ndimara@yahoo.com
www.ndimara.blogspot.com
NAOMBA KUWASILISHA