TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
OCTOBA 14, 2012
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inachukua fursa hii kumuenzi baba wa taifa “Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” wakati Tanzania inaadhimisha miaka 13 ya kifo chake. Juhudi za mwalimu katika kuleta maendeleo ya michezo pamoja na haki, usawa na ushirikiano kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutazienzi daima.
TPBC inakumbuka na kuenzi mchango wa baba wa taifa katika tasnia ya michezo hususan ngumi za kulipwa nchini tukikumbuka kuwa ni miaka ya mwisho ya utawala wake ndipo ngumi za kulipwa zilianza rasmi Tanzania mwaka 1982.
Juhudi za baba wa taifa za kuendeleza michezo zilikuwa na sura mbili kubwa:
Sura ya kitaifa: Michezo wakati wa utawala wa baba wa taifa ilianzia kwenye shule za msingi na kwenye vitongoji na hivyo kuwapa nafasi nzuri watanzania wengi wakati mzuri sana wa kushiriki na kuchangia kwenye maendeleo ya michezo.
Hii ilisaidia watanzania kujenga ari na vipani vya michezo ambavyo huanzia kwenye umri mdogo na hivyo kushiriki kwao kwenye michezo kuanzia shule za msingi na vitongoji kuliwapa nafasi nzuri ya kujijenga kimichezo.
Umri mzuri unaotakiwa kuanza kujishughulisha kwenye michezo ni kuanzia miaka 7 na kuendelea. Mtu anapoanza kujishughulisha kwenye michezo mapema akiwa na umri mdogo huweza kuonyesha na kuendeleza kipaji chake mapema na kwa hali ya juu.
Baba wa taifa alijenga msingi wa umoja na usawa ambao uliwezesha watanzania wote kushiriki katika michezo bila ubaguzi wa ukabila, udini na jinsia jambo ambalo halikuwa rahisi kwa nchi nyingine wakati ule.
Sisi tumejionea miaka ya karibuni kwenye michezo ya Olimpiki iliyomalizika katika jiji la London, Uingereza baadhi ya wanamichezo wa jinsia moja ndipo waporuhusiwa.
Hivyo baba wa taifa aliwezesha watanzania wote kushiriki kwenye michezo bila ubaguzi.
Sura ya Kimataifa: Serikali ya baba wa taifa ilijenga msingi imara kwa vyama vya kitaifa vya Tanzania kujiunga kwenye na mashirikisho mengi ya kimataifa kama vile CECAFA, Olimpiki, FIFA, AIAA, IBF, WBC, WTA na mengine mengi.
Uanachama huu watanzania kwenye mashirikisho haya uliweza kujenga misingi ya “Utalii wa Michezo” kwa Tanzania kujulikana duniani na hivyo kuwezesha nchi kutangaza vivutio vyake vya utalii na mahala pazuri pa kuwekeza.
Ni wakati wa utawala wa baba wa taifa mchezo wa riadha uliweza kuitangaza sana Tanzania katika medani ya kimataifa.
Jambo hili halina budi kuigwa na kuendelezwa na awamu zilizomfuata mwalimu hususan awamu ya sasa.
Sisi tunafikiri kuwa wakati rais wa sasa wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kiongozi wa kwanza mbali na mwalimu kuwekeza juhudi zake binafsi katika kuendeleza michezo, wale waliopewa jukumu la kusimamia tasnia hii hawana budi kumsaidia kuzifanya juhudi hizi zizae matunda.
Tunachukua fursa hii adimu ya kumuenzi baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika juhudi zake za kuendeleza michezo katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uongozi wa TPBC ni:
Rais: Onesmo Alfred McBride Ngowi
Makamu wa Rais: Godfrey Madaraka Nyerere
Katibu Mkuu: Nemes Kavieshe
Katibu Mkuu Msaidizi: Nicholus Mallya
Mwenyekiti wa Viwango na Ubingwa: Boniface Wambura
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji: Mark Hatia, Henry Mfinanga, Michael Buchato,
Imetolewa na Uongizi:
Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais,
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.