Mwili wa aliyekuwa
Kamanda wa jeshi la Polisi Mwanza, Marehemu Liberatus Barlow utaondoka katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando saa 1:00 asubuhi ya leo na kupelekwa nyumbani alikokuwa
akiishi marehemu eneo la Pasiansi jirani na kotaz za Marine Service.
Baada ya kufikishwa
kwenye makazi hayo mwili huo utakaa kwa muda wa dakika 30 kisha utapelekwa
viwanja vya Michezo Nyamagana ambapo kuanzia saa 2:30 Fursa itatolewa kwa
viongozi wa kada mbalimbali na wananchi kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza na
mikoa jirani kutoa heshima zao za mwisho kwa mchapakazi huyu aliyeiaga dunia
katika mazingira ya kutatanisha.
Baada ya zoezi hilo
kukamilika kwa nafasi yake mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow
utaondolewa kwa msafara hadi Airport Mwanza ambapo utasafirishwa kwenda nyumba
ya marehemu jijini Dar es salaam ambako familia yake inaishi.
Kesho (jumanne) zitafanyika lojistics mbalimbali ikiwa ni
pamoja na Maofisa wengine wa
jeshi la polisi Makao makuu (jijini Dar es salaam), wananchi, majirani na marafiki kutoa
heshima za mwisho kwa marehemu Kamanda Barlow, kisha mwili utasafirishwa
kuelekea mkoani Kilimanjaro hatimaye Marangu kijijini kwao kwa mazishi
yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumatano.
Kwa hivi sasa viongozi
mbalimbali wamekwisha wasili jijini hapa kwaajili ya taratibu za leo tangu juzi
tunaye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi, tunaye pia mkurugenzi
wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI Robert Manumba na timu yake, viongozi
wengine ambao walikuwa kwenye mbio za mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga Mh. Asha
Rose Migiro na wengine wengi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.