ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 4, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA DINI KUIMARISHA AMANI NA MAADILI NCHINI

▪️︎ Asema dini ni nguzo muhimu ya malezi na mshikamano wa Taifa

▪️︎ Asisitiza jamii kuendelea kuombea na kulinda amani ya nchi


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za dini nchini ili kuimarisha maadili, mshikamano wa kijamii na kudumisha amani ambayo ni msingi wa maendeleo endelevu ya Taifa.


Amesema hayo leo Jumapili, Mei 3, 2026, aliposhiriki ibada katika Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mufindi, lililopo Mafinga Mjini, mkoani Iringa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment