
Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga nchini Tanzania imeendelea kuthibitisha ukubwa wake, safari hii ikichezwa katika mazingira ya kipekee, kwenye uwanja wa kambini ama jeshini, Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
Sare ya mabao 2-2 haikuwa tu matokeo, bali ilikuwa picha halisi ya ushindani, ubora na presha ya mechi kubwa. Simba walianza kwa kasi na dhamira ya wazi ya kutawala mchezo mapema. Mabao ya Libasse Gueye na Clatous Chama yaliwapa faida ya mapema na kuonyesha mpango wao wa kushambulia kwa nguvu.
Lakini Yanga walirejea kwa utulivu na uzoefu. Kupitia Prince Dube na nahodha Bakari Mwamnyeto, walionyesha uthabiti na kupambana hadi dakika ya mwisho, japo matokeo yalisalia kuwa sare.
Sare hiyo inaacha pengo la alama tano likiendelea kuwepo, lakini zaidi ya hilo, imeacha mjadala mpana kuhusu kiwango cha dabi, mazingira ya mchezo na mchango wa wachezaji binafsi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment