Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kafiti William Kafiti ametembelea na kukagua eneo la Ujenzi wa jengo la kisasa la Abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza.
Katika Ziara iliyofanyika Leo Mei 19,2026 Kafiti, Amesema Ujenzi huo utasaidia Kiwanja cha ndege cha Mwanza kuwa na Jengo la Kisasa la Abiria lenye uwezo wa kuhudumia ndege zote za ndani na za nje ya Nchi.
Amebainisha kuwa Upanuzi wa kiwanja hicho utasaidia kukamilisha mahitaji ya Wananchi wanaotumia uwanja huo Kutokana na uwanja huo kuwa kilio Cha wakazi wa Mwanza Kwa Muda mrefu.
Katika hatua nyingine amesema Kukamilishwa Kwa Ujenzi wa jengo la kisasa la Kuhifadhia mizigo katika Kiwanja hicho kutarahisisha Shughuli za kiuchumi kama vile uvuvi, Viwanda na Biashara huku Kiwanja hicho kikipata Fursa ya kupokea ndege za kimataifa za mizigo kutokana na Jengo hilo kuwa na uwezo wa kupokea zaidi ya Tani 52,000 Hali itakayoinua uchumi wa Mkoa wa Mwanza na Nchi Kwa Ujumla.
Kwa Upande wake Meneja wa Uwanja wa ndege Mwanza, Rose Comino amempongeza Mbunge huyo Kwa kukipambania kiwanja hicho huku akibainisha kuwa kukamilisha Kwa jengo hilo kutawezesha utoaji wa huduma Kwa ndege za kimataifa na zaidi ya Abiria milioni mbili Kwa Mwaka.Kwa mujibu wa Kafiti William Kafiti, Mbunge wa Jimbo la Ilemela amesema Ujenzi wa jengo hilo la Abiria unatarajia kuanza mapema mwezi Julai.
Tupe maoni yako
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
0 comments:
Post a Comment